Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sam Elagalloor (katikati), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa zawadi mbalimbali zikiwemo shilingi milioni 50 zitakazotolewa na kampuni yake kwa wateja. Kushoto kwake ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Rahma Mwapachu, na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, wakiwa makao makuu ya ofisi hizo Barabara ya Morocco, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Jackson Mmbando (kushoto), akifafanua jambo.
Rahma Mwapachu akionyesha simu zitakazotolewa miongoni mwa zawadi katika mchakato huo.
Maofisa hao wa Aitel wakionesha zawadi zitakazoambatana na shilingi milioni 50 zitakazotolewa.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
Airtel yasherehekea Miaka 50 ya uhuru kwa namna pekee
·Wateja million 50 sasa
· Zawadi zenye thamani ya shilling million 600 kutolewa
·zaidi ya washindi100,000 kuzawadiwa tablets, simu na pesa tasmilim ndani ya siku tisini
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa mtandao mpana ulioenea zaidi, wenye huduma za bei nafuu inasherehekea miaka 50 ya uhuru kwa namna ya pekee ambapo katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru, Airtel imezindua promosheni kambambe itakayowawezesha wateja wa Airtel kujishindia zawadi zenye thamani zaidi ya shilling million 600.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Dar es Salaam, Mkurungenzi mkuu wa Airtel Tanzania Bw. Sam Elangalloor alisema, “katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru tumefikiria njia bora ya kuwazaidia wateja wetu na kuamua kuwazawadia zaidi ya shilling million 600 ikiwa ni zawadi mbalimbali na pesa taslimu katika msimu huu wa sikukuu, Zawadi tutakazotoa ni pamoja na muda wa maongezi , Modems, simu , Samsung Galaxy tablets pamoja na zawadi za pesa taslimu ambazo zitazawadia kwa wateja wetu wote walioko nchi nzima”
“Leo tunazindua promosheni yetu kambambe ya Mzuka wa Airtel kuadhimisha sherehe za uhuru ambapo wateja zaidi ya 100,000 wa Airtel watapata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali katika promosheni hii, kutakuwa na washindi 1020 wa kila siku watakaojishindia muda wa maongezi na simu, washindi 50 wa wiki watajishindia Samsung Galaxy Tablets na washindi wakuu 3 watajishindia zawadi za pesa taslimu shilling million 50. Tunafurahi sana kwa sababu shamrashamra hizi zimekuja wakati Airtel pia tunasherehekea mafanikio tuliyopata ya kufikisha wateja million 50 Afrika” aliongeza Elangalloor.
Aidha Menaja masoko wa Airtel Rahma Mwapachu alieleza njia zitakazotumika katika promosheni ya Mzuka wa Airtel, nakusema ” kujiunga na promosheni hii wateja wa Airtel wanatakiwa kutuma tu sms moja yenye neno MZUKA kwenda namba 15565.
Hakuna gharama zozote zitakazotozwa wakati wa kujiunga, wateja watajiongezea point na kupata nafasi ya kushinda pale ambapo watanunua muda wa maongezi kwa njia ya voucher za kukwangua au EVD Elecetonic Voucher nakuongeza salio katika simu zao, mteja atajikushanyia points kila wakati atakapo weka muda wamaongezi na kujiongezea nafasi ya kupata kujishindia zawadi mbalimbali katika kusheherekea miaka 50 ya uhuru wakati huu wa msimu wa sikukuu. Promosheni ya Mzuka wa Airtel, itadumu kwa muda wa siku 90 kuanzia leo 5th Desemba 2011.
Promosheni ya Mzuka wa Airtel, ni kwa wateja wote wa malipo ya awali, kadri mteja atakavyo weka muda wa maongezi na kuutumia ndio jinsi atakavyopata nafasi zaidi ya kuwa mshindi wa siku, wiki au mshindi wa droo ya kubwa.
Promosheni hii kubwa na kabambe ya Mzuka wa Airtel, ni kielelezo thabiti kinachoonyesha dhamira ya Airtel Tanzania katika kuzawadia wateja wake.
Ni siku kumi tu mpaka sasa ambapo Airtel imesherehekea mafanikio makubwa iliyoyapata kwa kujipatia wateja million 50 Afrika. Airtel imepata mfanikio hayo katika kipindi cha mienzi 17 tangu ilipoanza shughuli zake za biashara katika nchi 16 Africa na kuweza kuongeza wateja wapya wapatao million 14 katika kipindi hicho.
0 comments:
Post a Comment