Social Icons

Thursday, December 8, 2011

MALTA GUINNESS KUDHAMINI SIKU MOJA YA MAZOEZI YA VIUNGO DAR.

Meneja wa Kinywaji cha Malta Guinness, kinachozalishwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Maurice Njowoka akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam leo.

KAMPUNI ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Malta Guinness Desenba 8 mwaka huu itadhamini siku moja ya mazoezi ya viungo itakayokwenda kwa jina la ‘MALTA GUINNESS GOONESS DAY’ katika viwanja vya posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 4.

Mazoezi hayo yatajumuisha ’vituo vya mazoezi’ vya jijini Dar es Salaam ambapo mtaalamu wa mazoezi ya viungo atatoa mafunzo mbalimbali na namna ya kufanya mazoezi bora.

Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa Malta Guinness Bw. Maurice Njowoka amesema, kampuni hiyo imedhani siku hiyo maalum kama sehemu mojawapo ya kuihamasisha jamii kujijengea tabia ya kufanya mazoezi ili kuboresha na kuimarisha afya zao.

Njowoka amesema kuwa kampuni imekuwa na desturi ya kutoa huduma mbalimbali kwa jamii ya Tanzania kama sehemu ya mchango wake katika kuisaidia serikali katika kupambana na umasikini na maradhi na kujiletea maendeleo bora kwa watanzania wenye afya.

Akizungumzia kinywaji cha Malta Guinness, Njowoka amesema kampuni ya bia ya Serengeti imedhamini siku hiyo ya mazoezi ya viungo kupitia Malta Guinness kwa sababu ya sifa na ubora uliotukuka wa kinywaji hicho kutokana na ukweli kuwa Malta Guinness haina kilevi na pia hurudisha nguvu inayoweza kupotea wakati wa shughuli/kazi za kutumia nguvu na akili kama mazoezi ya viungo.

“Kampuni yetu kupitia Malta Guinness inayo furaha kuona wateja wake na watanzania wote wanaopenda maendeleo wakishiriki kikamilifu katika mazoezi kutokana na ukweli usiopingika kwamba mazoezi ndio tiba ya kwanza ya mwili wa binadamu, kwa sababu hiyo naomba ni chukue fursa hii kwa niaba ya Serengeti Breweries kupitia Malta Guinness kuwahamasisha watanzania wote wajijengee tabia ya kupenda mazoezi kwani mazoezi ni afya,”alisema Meneja wa kinywaji hicho Njoka.

0 comments: