Social Icons

Friday, December 9, 2011

DKT. BILAL ANOGESHA MKESHA WA MIKA 50 YA UHURU MNAZI MMOJA
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Koba, baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria Mkesha wa Sherehe za Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.

Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.

Wanenguaji wa Bendi ya TOT Plus, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.

Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.

Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.

Baadhi ya Vijana waliohudhuria sherehe hizo.



0 comments: