Meneja wa Tigo mkoa wa Morogoro, Noel Maktauwa (kulia) akikabidhi vitabu kwa mwakilishi wa makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dkt. Adam Mwakalobo (katikati). Kushoto ni Dr. Rex Kidyalla ambaye ni mkurugenzi wa Maktaba chuoni hapo. Tigo ilikabidhi vitabu pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya fainali za mashindano ya Tigo Inter-College yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Dkt. Rex Kidyalla ambaye ni mkurugenzi wa Maktaba katika Chuo Kikuu cha Dodoma akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano ya Vitabu kutoka kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo iliyofanyika hivi karibuni chuoni hapo. Katikati ni mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo hicho Dkt. Adam Mwakalobo. Kulia ni Meneja wa Tigo mkoa wa Morogoro, Noel Maktauwa. Tigo ilikabidhi vitabu pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya fainali za mashindano ya Tigo Inter-College yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Rogers Lucas akitoa burudani mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika juzi chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Nick Wa Pili akitoa burudani mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika juzi katika Ukumbi wa Club La aziz chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo.
Taarifa Kwa Vyombo Habari
Informatics washindi Tigo Inter-College UDOM
Tarehe 4 Desemba 2011, Dodoma.
TIMU ya soka ya College of Informatics and Virtual Education ya chuo kikuu cha Dodoma, juzi iliibuka mabingwa wa mashindano ya Tigo-Inter-colleges yaliyofikia kilele chake katika viwanja vya Chuo Kikuu hicho mjini Dodoma, baada ya kuwafunga wenzao wa College of Health Sciences kwa bao 1-0 katika mechi ya fainali.
Halikadhalika katika mchezo wa kikapu timu ya Informatics and Virtual Education iliwabukiza tena College of Health Sciences kwa jumla ya vikapu 43-37 katika mchuano wa fainali pia. Mashindano hayo yalishirikisha vyuo vilivyoko chini ya Chuo kikuu cha Dodoma.
Mechi ya soka ilikuwa ya upinzani wa hali ya juu kutokana na viwango vilivyoonyeshwa na timu zote. Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionyesha hali ya kukosa nafasi ya kupata magoli dhidi ya mwenzake. Goli la ushindi la Informatics lilitiwa kimiani na mchezaji Sidne Mbele baada ya kuiadaa ngome ya College of Health Science kabla ya kukwamisha mpira wavuni.
Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika katika chuo kikuu hicho kwa muda wa siku sita chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. Washindi wa michuano hiyo wote walikabidhiwa vikombe.
Awali fainali hizo ziliambatana na makabidhiano ya vitabu kutoka kampuni ya Tigo kwa uongozi wa chuo hicho ambapo mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma, Dkt. Adam Mwakalobo aliishukuru kampuni ya Tigo kwa kusaidia chuo hicho na pia kudhamini michezo chuoni hapo.
Mashindano hayo ambayo yaliambatana na sherehe maalum ya kuwakaribishwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo iliyofanyika jioni baada ya kukamilika kwa mechi za fainali chuo hapo, yalikuwa yamegawanya timu katika makundi mawili, kwa kila kundi kuwa na timu nne.
Kundi A lilikuwa na timu za School of Curriculum and Teacher Education, School of Education Studies, College of Earth Sciences, College of Natural and Mathematical Sciences. Kundi B lilikuwa na timu za School of Social Sciences, School of Humanities, College of Informatics and Virtual Education, College of Health Sciences.
0 comments:
Post a Comment