Kama kawaida, wabunge wa Chadema na wa NCCR Mageuzi wamesusia kikao cha kujadili mchakato wa kuunda katiba mpya na kuamua kutoka nje, mara baada ya Tundu Lisu kuwasilisha mapendekezo ya kambi ya upinzani. Ilitolewa mionngozo juu ya hoja kadhaa zilizojitokeza lakini spika alizikataa na ndipo wabunge hao wakaamua kutoka nje na kuacha wabunge wa ccm na wengine kama TLP kuendelea na kuchangia mapendekezo yaliyotolewa na Waziri wa Katiba, Mama Kombani.
Majadiliano yataendelea kesho kama kawaida kwa wabunge kuujadili mswada huo kwa mara ya pili kwa mujibu wa taratibu na kanuni za bunge ambazo zimeonekana kupotoshwa na wanaharakati. Watu wengi wameelewa kuwa kilichokuwa kifanyike leo ni kujadili muswada wa katiba mpya hivyo usomwe kwa mara ya kwanza ili watu wauelewe na watoe maoni yao, wakati kumbe kinachojadiliwa ni namna ya kuandaa utaratibu wa kuunda hiyo katiba mpya na namna ya watu kupewa nafasi ya kutoa maoni na madukuku yao kuhusu katiba hiyo ijayo!!
0 comments:
Post a Comment