Sugu akiongea na wanahabari kwa msisitizo (kulia) ni Zay B, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki wa Kundi la Vinega.
Sugu akionesha kitabu cha historia ya maisha yake kutoka mtaani mpaka bungeni, kiitwacho Muziki na Maisha.
MBUNGE wa Mbeya mjini na msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo asubuhi aliwaongoza wasanii wenzake anaotarajia kutoa burudani ya nguvu kwenye Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Jumamosi ijayo katika mkutano na wanahabari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari ‘Maelezo’.
Kundi la wasanii hao linalojiita Vinega limeahidi kufanya makamuzi ya aina yake kwenye onesho hilo ambalo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi.

Hard Mad akionesha tabasamu baada ya kufurahishwa na maneno ya Sugu.

Msanii wa Mabaga Fresh, DJ Snox akionesha vionjo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).

D wa Gheto naye ni miongoni mwa wanamuziki wa Kundi la Vinega walioahidi kufanya kufuru kwenye onesho hilo.

Baadhi ya wasanii wanaotarajiwa kufanya makamuzi wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.

0 comments:
Post a Comment