Social Icons

Tuesday, November 22, 2011

TWANGA PEPETA KUKAMUA LONDON WIKI HII

Mkurugenzi wa Bendi ya African Star International (Twanga Pepeta), Asha Baraka (kushoto) akionyesha moja ya DVD feki za albamu mpya ya bendi yake iitwayo ‘Dunia Daraja’


BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars International “Twanga Pepeta” itafanya onyesho kwa mara ya pili nchini Uingereza Jumamosi hii.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, alisema kuwa jumla ya wasanii 13 wanatarajiwa kwenda huko kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru na Watanzania waishio huko.

Baraka alisema wanamuziki wao wanatarajiwa kuondoka Ijumaa na shoo itafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Silver Spoon, Wembley.

Mara ya kwanza kwa bendi hiyo kufanya shoo London ilikuwa mwaka 2007 ambapo ilifanya maonyesho kwa wiki tatu katika miji mbalimbali.

Alisema mgeni rasmi katika shoo hiyo anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania wa Uingereza ambaye ni Peter Kallaghe. Baraka aliongeza kwamba maandalizi ya safari hiyo yanaendelea vizuri.

“Kwa vile Watanzania tulitawaliwa na Waingereza na kuna Watanzania wanaoishi huko, tumeona ni vyema tukaenda kuungana na wenzetu kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya uhuru, alisema Baraka.

“Wasanii wanaoenda huko ni 13 na wengine watabaki kuendelea na shoo kama kawaida kwenye kumbi mbalimbali katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na tutaungana pia na Msondo Ngoma katika burudani hiyo,” alisema Baraka.

0 comments: