CHADEMA YAJIFARIJI KITI KIMOJA CHA UDIWANI ENDASAK!!!
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeshinda kiti kimoja cha Udiwani katika Kata ya Endasak, ambako ni nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mary Nagu ambaye pia ndiye Mbunge wa Jimbo la Hanang ilipo kata hiyo.
Ushindi huo wa Chadema sasa unakifanya chama hicho, kuwa na idadi sawa ya madiwani na CCM katika Halmashauri ya Hanang kwa kufikisha madiwani 12. Pia kila chama kina mbunge mmoja, Nagu na Rose Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema).
Kwa mujibu wa matokeo kutoka vituo 13 vya kura, mgombea wa Chadema, Hashim Muna alipata kura 1,244 wakati mgombea wa CCM, Lazaro Shauri alipata kura 1,183. Kura 62 ziliharibika.
0 comments:
Post a Comment