Chiby Dayo, ambaye amewahi kuwa kwenye Danger Zone ya shindano hilo zaidi ya mara nne sasa bila kutolewa, jana alifikwa na makubwa jukwaani wakati wa kurekodi kipidi cha shindano hilo, SORYY,kukufunulia hii kwa sasa siwezi kutokana na utaratibu wa uongozi wa shindano hilo, ila kwa kupata tukio zima ni vizuri ukafuatilia kipindi hicho Jumamosi hii mishale ya saa 3: 30 usiku ITV. SORRY KAMA NIMEKUKWAZA LEAVE ME ALONE!!!
Mshiriki wa shindano hiloChiby Dayo, akiwa chini mara baada ya kutajwa matokeo ya aliyeenguliwa kwenye tano bora. Washiriki walioingia kwenye tano bora wakiwa katika pozi la pamoja muda mfupia baada ya kutajwa aliyetoka kwa wiki hii, huku Chiby Dayo akiwa amejiinamia chini. Washiriki hao wakiserebuka na watangazaji wa kipindi hicho Godwin Gondwe (wa pili Kushoto), na Bob Junior aliyeshika ‘mic’ (kushoto), katika Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, mara baada ya kuhitimisha shughuli za kuandaa kipindi hicho.
Jaji mkuu wa shindano hilo Lita Paulsen ‘Madam Lita,’ akiteta jambo na muongozaji mkuu wa kipindi hicho (mbele yao), na Salama Jabir jana Mbalamwezi Beach.
Washiriki walioingia kwenye tano bora wakiwa katika pozi la pamoja muda mfupia baada ya kutajwa ataliyetoka kwa wiki hii
: Mshindi wa shindano la Tusker Project Fame, 2011 Peter Msechu (wa kwanza kushoto), akifuatiliamchakato huo na Mshindi mwenzake wa Project Fame Alpha (wa pili kulia), na marafiki zao.
Mshiriki wa BSS 2nd Chance 2011 Haji Ramadhan, akiwajibiki jukwaani hapo.
Rogers Lucas akichalaza gitaa kutetea nafasi yake.
Waziri Salum, akiwajibika.
Bella Kombo, akitetea nafasi yake.
Mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa shindano hilo Imani Lissu, akishuhudia mchakato mzima mahali hapo.
WASHIRIKI wa shindano la kumsaka mwenye kipaji cha kuimba la Bongo Star Search Second Chance 2011, hatimaye linazidi kufikia patamu ambapo sasa washiriki walioingia kwenye tano bora ya shindano hilo, wanazidi kubanana vilivyo kufuatia kila mmoja kuhitaji kunyakua kitita cha shilingi Milioni 50 zilizotangazwa kuchukuliwa na mshindi wa kwanza wa shindano hilo.
Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye tano Bora ni Chiby Dayo, Haji Ramadhan, Rogers Lucas, Waziri Salum na Bella Kombo.
Washiriki hao wanatarajiwaSeptemba 24 mwaka huu ndani ya jiji la Mwanza kwaajili ya kufanya shoo ya utangulizi kabla ya siku ya fainali ya shindano hilo kuifikia na jumapili hii ya septemba 26 watamalizia mjini Arusha.
0 comments:
Post a Comment