Social Icons

Thursday, September 22, 2011

MASTAA BONGO KUONYESHANA NYONGA NA TWANGA PEPETA JUMAMOSI HII MANGO GARDEN Baadhi ya wanenguaji wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani' wakiwa katika pozi la pamoja.
Wanenguaji wa bendi hiyo katika pozi.
Hawa ni moja wa masta watakao hudhuria siku hiyo kushoto Latifa Idabu 'Badra', akiwa na Skyner Ally (katikati), na Rafiki yao.
Msanii ndani ya kiwanda cha filamu Bongo, Irene Uwoya 'Oprah' katika pozi.
Msanii wa vichekesho Bongo, Hussein Mkieti 'King Sharo- milionea, Rais wa Maswaga'.

Na Shakoor Jongo/Mateja20

BENDI ya muziki wa dansi nchini African Stars, ‘Twanga Pepeta’ imeandaa shoo maalumu kwa ajili ya kuwashukuru masupastaa wote wa Bongo wanaoiunga mkono bendi hiyo.

Onesho hilo litakalofanyika ndani ya Ukumbi wa Mango Garden uliopo jiijini Dar es Salaam Jumamosi Septemba 24, mwaka huu, onesho hilo limepewa jina la Usiku wa Mastaa ambapo kionjo cha habari hii kimetolewa na Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka.

Mwanadada huyo amewajulisha wadau wa muziki nchini kuwa, bendi yake imeamua kufanya shoo hiyo kwa lengo la kushukuru mchango wa watu maarufu kwa bendi yake.

“Burudani bila mastaa hainogi…tunajua kuna watu wanahudhulia shoo zetu kwa sababu ya kuwaona masupastaa, kwetu sisi uwepo wao ukumbini ni mchango mkubwa,” alisema Asha.

Akielezea utamu utakaopatikana kwenye onesho hilo Asha alisema, bendi yake itaungurumisha muziki na shoo ya nguvu huku nafasi ya kushambulia steji kwa nyonga na makeke ikiachwa wazi kwa masupasta. Shoo hiyo itakuwa na kiingilia kidogo.



0 comments: