Social Icons

Wednesday, September 7, 2011

WATANZANIA WENZANGU TUMSAIDIE MZEE KIPARA


JE, UNAMFAHAMU muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la ‘Mzee Kipara?” Kama jibu ni ndiyo basi soma habari hii na kisha kuwa muungwana huku ukijua kuwa Imani ni moyo wa kujitokea.

Mzee Kipara ambaye jina lake halisi ni Saidi Fundi (pichani) hivi sasa anasumbuliwa na miguu kukosa nguvu, tatizo ambalo endapo atapelekwa hospitali pengine linaweza kupata nafuu kama si kupona kabisa.

Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa.

Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi.

Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake wataweza kumsaidia kwa hali na mali.

“Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha,” alisema Kuyunga.

N.B. Kutoa ni moyo na siyo utajiri, hivyo hima popote ulipo nchini, msaidie mzee huyu kwa kumtumia kiasi chochote utakachojaaliwa kwa njia ya M-PESA AU TIGO PESA, itamfikia mwenyewe moja kwa moja na unaweza kuongea nae kwanza.

0 comments: