Social Icons

Wednesday, September 7, 2011

UNFPA YAENDESHA SEMINA YA AFYA YA UZAZI KWA WAANDISHI WA HABARI DK. Elizabeth Mapela kutoka Wizara ya Afya kitengo chaAfya ya Uzazi na Watoto, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema kabula ya semina ya Waandishi wa habari kuanza ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Protea mapema leo jijini Dar es Salaam.
Mhariri kutoka kampuni ya Global Publishers LTD Hamida Hassan, akielezea jambo kwenye semina hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wadau wengine waliyohudhulia semina hiyo wakisikiliza maada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa mambo ya habari kutoka Femina Amabilis Batamula, akisikiliza moja ya swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi wa habari waliyokuwepo mahari hapo.
Meneja wa Mradi wa Ukimwi na Ulemavu CCBRT Clement G Ndahani, akiongea jambo katika semina hiyo.
Mtaalam wa Masuala ya UKIMWI na Vijana kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la (UNFPA) Dk Chilanga Asmani, akitoa mada kwa waandishi wa habari waliyohudhulia semina hiyo kuhusu Afya ya uzazi salama kwa vijana na jinsi ya kupata mbinu za kujikinga na maambukizi ya ukimwi, katika semina iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Protea jijini Dar es salaam Tanzania.
Wadau mbalimbali katika semina hiyo wakijadili jambo wakati wa semina hiyo (kutoka kulia ni), Ofisa Habari wa UNFPA Sawiche Wamuza, Kyoko Shimamoto kutoka UNFPA, John Ambrose kutoka Asasi ya Adolescent Psychosocial consultancy Services (APCS) na Dr Elizabeti Mapella kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya wadau waliyohudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makini baadhi ya mambo yaliyokuwa yakiendelea mahali hapo.
Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mchakato huo.
Mtoa Mada kutoka Femina, Amabilis Batamula, akizungumza jambo mahali hapo.
Baadhi ya watoa mada waliyohudhulia mahari hapo wakijadili jambo.
Dr. Dr. Chilanga Asmani na Kyoko Shimamoto kutoka UNFPA wakijadili jambo wakati wa semina hiyo.
Baadhi ya wanahabari hao wakifuatilia kwa makini zaidi mchakato huo.


0 comments: