Social Icons

Friday, September 23, 2011


MAD ICE KUWAPIGA JEKI WASANII WA KIBONGO


Na Erick Evarist


MSANII wa longtime ndani ya gemu la muziki wa kizazi kipya nchini, Mad Ice juzikati aliahidi kuwasaidia wasanii kibao wa kibongo kulisongesha mbele gurudumu la muziki wa Bongo Fleva.

Akipiga stori mbili tatu na Paparazi wetu hivikaribuni maeneo ya Millenium Towers Kijitonyama jijini Dar es Salaam, alisema kwamba mara atakapo rejea maskani kwake anakuishi kwa sasa nchini Finland, atahakikisha anatangaza kazi mbalimbali za kimataifa kupitia mtandao wake na wabongo wengi watapata kutangaza kazi zao kupitia mtandao wa kampuni hiyo.

“Nimegundua kuna vipaji vingi sana kwa wasanii wa hapa nyumbani kwa mfano ukiangalia kazi za Linex utagundua kabisa vijana wa sasa wanajituma kwani hata kama wimbo una ujumbe wa mapenzi lakini si ili mradi tu mapenzi lakini kuna kitu flani spesho ndani yake.

“Kuna vipaji vingi chipukizi ambavyo tukiungana na kujitangaza pamoja katika soko la kimataifa nadhani tutafika tunapohitaji maana kama kazi ya msanii itakuwa nzuri ataweza kuitwa popote kwa ajili ya shoo na mambo mengine ya kuelimisha jamii kupitia sanaa yake,” alisema Mad Ice.

Utaratibu mzima wa namna ambavyo wasanii watatakiwa kutuma kazi zao sikilizia hapa hapa tutakulisha.

0 comments: