Social Icons

Friday, September 9, 2011


MARY LUCAS, SHAFII ZUBERY MAPENZI YATAWALA BSS 2011.


MSHIRIKI wa BSS 2010, Shafii Zubery, juzikati alimwibukia anayedaiwa kuwa mpenzi wake ambaye ni mshiriki wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, Mary Lucas, mjengoni humo.

Ishu hiyo ilijiweka wazi Septemba 7 mwaka huu ndani ya Fukwe za Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki hao walikuwa kwenye mchakato wa kuandaa kipindi hicho kinachorushwa hewani kila siku ya jumamosi katika kituo cha ITV.

Wakiwa katika mchakato huo, washiriki hao muda mwingi Mary alionekana kuwa bize na Shafii suala lililomfanya Paparazi wetu, kutaka kujua ni kipi kinachoendelea pande hizo.

Paparazi wetu baada ya kufika hapo aliwahoji Mary na Shafii juu ya ukaribu huo, kutokana na majibu yao alibaini kweli ni wapenzi na kwamba Shafii alitoka Dodoma kuja Dar kwaajili ya kumsapoti kipenzi wake huyo na alikuwa na haya ya kusema.

“Kwani ni kipi kisichojulikana kati yangu na Mary mbona wengi wanajua na kama ulikuwa haujui basi itakuwa ulichelewa sana na unatakiwa uongee na Haji Ramadhani au Chiby Dayo, hao watakufahamisha zaidi”. Alisema Shafii.

Kwa upande wa Mary yeye hakutaka kuzunguka hivyo alikili moja kwa moja kuhusiana na ukaribu wao kwa kusema kwamba, “ Huyu ndiye Mr, wangu na hakuhitaji swali maana kama maswali tulishayajibu sana na sasa kinachotakiwa kuangaliwa zaidi ni upendo tu, maana sasa tunakoelekea mapenzi yetu yameshapitiza na tumezoeweana kama mtu na dada yake” Alisema Mary Lucas ambaye pia ameyaaga mashindano hayo.

0 comments: