Social Icons

Friday, September 9, 2011

KITALE: NITANG'OA MTOTO WA RAIS SIKU SI NYINGIWasnii wa vichekesho Bongo Sharomilionea (kushoto), akiwa katikapozi la kisanaa na Kitale.

MSANII katika Tasnia ya filamu Bongo, anayesimama vyema kwenye upande wa uchekeshaji Mussa Kitale, anadaiwa kuwa mlinzi hodari katika kambi yao iliyopo pande za Uyole mjini mbeya,
ambako kwa sasa wapo kwaajili ya kucheza filamu zao mpya na michezo kazaa ambayo itakuwa ikirushwa hewani na kituo cha Chanal Ten kila siku ya Ijumaa.

Akipiga stori na mateja20, juzikati tale alisema kwamba muonekano wake wa Kiteja ni kwenye sanaa tu lakini yeye hana tabia hizo kama watu wanavyomchukulia kila kukicha.

Tale, aliyesema hayo baada ya usumbufu mwingi kutoka kwa mashabiki wake wa pande hizo kuzidi kumgasi kila anapokutana nao.

"Kwakuweka wazi naomba mashabiki wangu waelewe kuwa mimi ni askali mwema ndani ya raia hata kambini kwetu, hivyo niko makini na sina chembechembe yoyote ile ya uteja, zaidi ya uteja wangu kuutumia katika sanaa tu", Alisema Tale, huku akitania kuwa siku chache zijazo atajitengenezea heshima zaidi maana anahitaji kung'oa mtoto wa Rais, kwani kupitia mchumba huyo heshima itapatikana tu.
Kitale, akionyesha swagger zake akiwa kwenye pozi husika la kuigizia.
Kitale na swagger la kimgambo zaidi.

0 comments: