'MCHUNGAJI MASANJA MKANDAMIZAJI WA ORIJINO COMEDI AKIWAJIBIKA JUKWAANI KUWAOMBEA WANA WA MUNGU'

Mchekeshaji maarufu kama Masanja Mkandamizaji, majina halisi Emmanuel Mgaya wa kundi la Ze Komedi Orijino ya TBC 1 inayorusha vichekesho vyao kila alhamis kuanzia saa moja usiku, amempa Yesu maisha yake na tayari muda mrefu ameonekana sehemu mbalimbali akiendeleza kipaji chake huku akihubiri na kuimba nyimbo za Injili na wengi wakimpa Yesu maisha yao.
Hivi karibuni alisikika kwenye kipindi cha redio moja maarufu kinachokuwa hewani kila jumapili kuanzia saa 12.30 alfajiri hadi saa 3.00 kikiongozwa na Mtangazaji, Mchungaji Harris Kapiga, Masanja alisema “Mimi ni mchungaji mtarajiwa lakini huduma yangu ya uchungaji nimeanzia kwenye kundi langu hili la Orijino Komedi, kupitia hilo nina washirika wangu ambao natamani wawe kama mimi mchungaji wao wafuate nyayo zangu, naomba maombi ya watumishi wengine wamuombee Joti” alisikika kwa msisitizo!
Kwa sasa, Masanja anaabudu kanisa la EAGT, Mito ya Baraka pia amefanikiwa kutoa nyimbo 10 za Injili na tayari album yake ya HAKUNA JIPYA iko mitaani!

0 comments:
Post a Comment