Social Icons

Monday, September 26, 2011

MASHABIKI WAFURIKA SHOO YA MASTAA NA TWANGA PEPETA, MANGO GARDEN Mwanamuziki wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani' Charles Gabriel 'Chalza Baba' (katikati), akiongoza safu ya wanenguaji wa bendi hiyo kusherehesha usiku huo na mastaa mbalimbali waliojitokeza ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mnenguaji machachali wa bendi hiyo Asha Said 'Sharapova' akiwajibiki jukwaani hapo.
Staa wa filamu Bongo Steven Charles Kanumba, akifungua Shampeni ndani ya ukumbi huo kama ishara ya upendo kwa mashabiki wa bendi hiyo na mastaa wote waliozama kwenye kiwanja hicho siku hiyo.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka (wa pili kulia), akifuatilia kwa makini namna wanamuziki na wanenguaji wake walivyokuwa wakiwajibika jukwaani hapo, wa kwanza kushoto ni Steveni Kanumba akitazama shoo hiyo mara baada ya ufunguzi wa shampeni kukamilika (katika yao), ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa bendi hiyo Karim Sospita.
Mnenguaji wa bendi hiyo Abilah Muzungu, akipanawisha mashabiki zake.
Mmoja wa mashabiki wa bendi hiyo akimfuta jasho mnenguaji wa bendi hiyo Abuubakari Kisongo 'Mandela.
Mwimbaji mpya wa bendi hiyo Venansi (kushoto), akiserebuka na mmoja wa mashabiki jukwaani hapo.

Mpiga Drums wa bendi hiyo Jemes Kibosho, akiwajibika.
Wanenguaji wa bendi hiyo wakitoa burudani kwa mashabiki wao.
Mashabiki waliojitokeza siku hiyo wakiserebuka ukumbini hapo
Mnenguaji wa bendi hiyo Maria Soloma, akiwajibika
Mwanamuziki wa bendi hiyo Saleh Kupaza (kulia), akisugua kisigino na shabiki wake.
Mashabiki walijinafasi namna hii.
Wanenguaji shughulini.
Ukumbi ulifurika namna hii.


BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ usiku wa kuamkia leo imefanya onesho maalum la kuwaburudisha mashabiki wake na mastaa mbalimbali katika Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam. Katika onesho hilo bendi hiyo ilitangaza uzinduzi wa albam yake ya 11 utakaofanyika Novemba 6 mwaka huu. Yafuatayo ni baadhi ya matukio yaliyojili kwenye onesho hilo.




0 comments: