Social Icons

Saturday, September 24, 2011

TUSKER LAGER YAZINDUA KAMPENI MPYA YA KUSHEREHEKEA UBORA NA URITHI WA KINYWAJI HICHO

KAMPUNI ya kinywaji cha bia ya Serengeti Lager (SBL), lkupitia kinywaji chake cha Tusker Lager, leo imezindua kampeni mpya ya kusheherekea ubora na urithi wa kinywaji hicho uuliyokuwepo tangu mwaka 1922 cha kinywaji hicho kilipoingia nchini.

Tusker kinywaji kinachozalishwa hapa nchini kwa vimelea vyenye asilimia 100, hadi leo hii inazidi kuonyesha uasilia wa kinywaji cha Afrika kwa 100%.

Kampeni hiyo itakayokuwa na hamasa za kipekee itahusisha Matangazo ya mvuto wa kipekee na ubalozi maalumu utakao wakilisha kinywaji cha Tusker na Matukio ya kipekee katika maeneo yote nchini, katika promosheni maalumu itakayojulikana kama Tusker ‘Life and Soul’.

Akijaribu kukielezea zaidi kinywaji hicho Mkurugenzi wa masoko Ephraim Mafuru alisema

“Tusker ambayo ni kinywaji pekee kilichokuwepo tangu wakati Tanzania ikipata uhuru wake mwaka 1961, kimeendelea kuwa na ladha yake ya kipekee na ubora wa aina yake tangu wakati huo”,

Mafuru aliongeza kuwa

“Tusker imekuwa kinywaji bora kwa wakati wote na kimekuwa kinywaji kinachoweza kutumika katika sherehe na hafla mbalimbali huku kikitumika kuwakusanyana kuwaweka pamoja watu wenye rika na hulka tofauti katika maisha ya kila siku”,

Promosheni ya kitaifa kwa wateja wote iliyomalizika hivi karibuni iliyojulikana kama ‘Tusker Milioni 500 kwa Mashabiki’ ilikuwa ya mafanikio makubwa ambapo zaidi ya watanzania 121 walijazwa mamilioni ya fedha.

“Tunajivunia kinywaji cha Tusker ambacho kupitia promosheni hiyo kimeweza kutengeneza mamilionea ambao kwa hakika fedha hizo zimeingia katika uchumi wa Tanzania.

Alisema kinywaji hicho pia kinajivunia udhamini wake katika shindano la Tusker All Stars ambapo Peter Msechu mwakilishi wa Tanzania alishiriki katika mashindano ya kimataifa yaliyofanyika Nairobi, Kenya wiki chache zilizopita.

Kwa upande wake, Meneja wa kinywaji hicho Rita Mchaki alisema “Kujihusisha kwetu katika matukio tofauti ya kihuduma katika taifa hili kunatupa ujasiri wa kujivuna na kutembea kifua mbele”.

Mchaki alisema kinywaji cha Tusker kitaendelea kusaidia mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika maeneo tofauti katika kuhakikisha jamii ya kitanzania inakuwa na maisha bora.

“Tuna furaha kushiriki na jamii ya kitanzania katika kampeni yetu mpya ambayo itaanza hivi karibuni.Tunaomba watanzania waangalie mara kwa mara matangazo yetu yatakayoanza kurushwa hivi karibuni”, alisema Ephraim Mafuru.

0 comments: