Mnenguaji wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani', Sabrina Mathew (kushoto), akikamua na mmoja wa mashabiki waliojitokeza kwenye onesho hilo ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar. Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakiwajibika jukwaani hapo. Kiongozi msaidi wa wanenguaji hao Lilian Internet, akiwajibika vilivyo mbele ya mashabiki wake. Kimwana Twanga Pepeta 2011, ambaye pia ni mmoja wa wanenguaji wa bendi hiyo Mary, naye akionyesha uwezo wake kwa mashabiki wake katika sikukuu ya Idd. Mmoja wa mashabiki wa bendi hiyo akiwa amejiachia katika pozi kwa aibu siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment