Social Icons

Friday, September 2, 2011

KEKI YA BIRTHDAY YA KIMWANA TWANGA PEPETA 2011, YAASHIRIA MAMBO MAKUBWAJANA ilikuwa siku ya Idd pili, ambapo Kimwana namba nne wa Twanga Pepeta 2011, Mariam Hamisi, alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge Kinondoni Mbuyuni jijini Dar es Salaam. Kilichoacha hoi baadhi ya waalikwa wake ni muonekano wa Keki aliyokuwa ameiandaa, maana ukiitazama vizuri muonekano wake ni kama umbile la mtu aliyevaa sindiria na chupi tu, kiukweli mimi pia sikuielewa zaidi ilimaanisha nini.
Huyu ndiye Mariam, ambaye alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake na kuandaa keki yenye muonekano huo, hapa amebeba keki hiyo tayari kwa kuwalisha wapendwa wake.
Mariam, akiwa kwenye pozi na rafiki yake ambaye jina halikufahamika mara moja muda mfupi kabla ya kukata keki hiyo.
Baadhi ya marafiki zake waliomsapoti kwenye sherehe hiyo wakiselebuka ukumbini hapo.
Mariam (kulia), akimlisha keki mmoja wa marafiki zake.
Mmoja wa washiriki wa Kimwana Twanga Pepeta 2011, Amina (kushoto), akilishwa keki hiyo.
Mnenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Bakari Kisongo 'Mandela', akiwa katika pozi nje ya ukumbi huo.
Mshiriki wa Kimwana Twanga Pepeta 2011, Dina, akipozi namna hiyo nje ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Eee! mambo ya Dina hayo....

0 comments: