Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya muziki wa Tanzania House Of Talent (THT), wakiwa kwenye pozi la pamoja na wageni waarikwa waliohudhulia mahali hapo muda mfupi baada ya kukamilisha shughuli ya upokeaji vyeti.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rugemalila Mutahaba 'Ruge', akiseti vyombo vya muziki mahali hapo.
Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family Saidi Fella (mbele), akidansi na kiongozi wa kundi la Tip Top Connection Babu Tale, katika tafirija hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa THT, Amini akicheza mduara mahali hapo.
Msanii Benald Paul 'Ben Pol' (wa pili kushoto), akiwa katika pozi na baadhi ya wahitimu wa mafunzo wa THT katika sherehe hizo.
Linah akiserebuka mahali hapo.
Asha Baraka akilisaka rumba mahali hapo.
Mh..! hapa Mwasiti akigombea keki na baadhi ya wadau.
...Akiwa na mashabiki wa muziki katika pozi.
... akimega keki hiyo baada ya kusogezewa karibu.
Miss Tanzania namba tatu 2011, Alexia William (kushoto), akiwa na mmliki wa Blog ya Uniquetz Bw. Magese (Kulia), na mmoja wa wadau.
Mwasiti akiondoka eneo hilo.
Mtangazaji wa Clouds Loveness Love 'Diva' akikwepa kamera ya Mateja20 baada ya kufumwa akipiga stori na wadau wa burudani mahali hapo.
Msanii kutoka THT anayefanya vizuri katika muzikiwa Kizazi Kipya Bongo, Esterina Peter Sanga 'Linah' akijianda kula keki kutoka kwa mmoja wa wasanii wenzake wa THT.
...Akiwa na miss Tanzania namba tatu Alexia William.WASANII kutoka jumba la kukuzia vipaji Tanzania, Tanzania House of Talent (THT) jana Septemba 18 mwaka huu walifanya mahafali
Wakati wahitimu zaidi ya 20 walipoingia katika Ukumbi huo walianza kushusha burudani mfululizo kuonesha kuwa wamepikwa wakapikika, burudani ya aina yake iliyodumu kwa takriban masaa mawili na nusu ilifana kwa kiwango kikubwa hasa pale wasanii hao walipokuwa wakiimba nyimbo zao pamoja na nyimbo za wasanii maarufu kutoka nje, hali iliyowafanya wageni waalikwa kupagawa na kupiga shangwe za kufa mtu.
Baada ya hapo lilifuatia zoezi la ufunguzi wa shampeni na baadaye mwanamuziki kutoka kiwanja, Bruno Mars aliimba ngoma tofauti tofauti za wasanii kutoka nje ya taasisi hiyo.
Wadau mbalimbali walipongeza ujio huo mpya wa THT kwani kila mtu aliamini ipo haja ya kuenzi nyimbo na tamaduni za asili ambazo pia zilifunika ile mbaya.
Wasanii kama Winfrida Josephat 'Rachl, Amini Mwinyimkuu Mpili 'Amini', Barnaba Elias 'Barnabai, Lina, Dito, Mwansiti, Wahitimu na kinda kutoka kwa mkubwa Fela, Ansley waliinua umati kwa shagwe walipopamda stejini.
Mahafali hayo ya pili kwa mwaka huu, yalifanyika tofauti hali iliyopelekea wadau wengi wa burudani kupongeza uongozi mzima unaoongozwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Ruge Mutahaba kwa kuweza kuwapika vijana kwa ajili ya kujipatia ajira.

0 comments:
Post a Comment