BSS 2nd CHANCE 2011 YAFIKIA PATAMU, BEATRICE WILLIAM AYAAGA MASHINDANO KWA UCHUNGU
Mshiriki wa kinyanga'nyiro cha Bongo Star Search Second Chance 2011, Beatrice Wiliam, akikamua siku ambapo walikuwa wakirekodi kipindi hicho muda mfupi kabla ya kutangazwa kuyaaga mashindano hayo, katika mchakato uliyofanyika kwenye Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam katika ya wikiliyopita.
Beatrice akiwajibika jukwaani hapo.
Mshiriki wa sindano la Bss Second Chance 2011, Haji Ramadhin akitetea nafasi yake kwa bidii zote siku hiyo, ambapo aliwaacha hoi majaji wa shindano hilo baada ya kuzungusha nyonga yake vilivyo.
Jaji wa shindano hilo Masta J (kushoto), akiangua kicheko huku akiwa amemkumbatia Jaji mkuu wa mchakato huo Madam Lita, wakati wa makamuzi ya Haji Ramadhan.
Salama Jabir (kulia), akimuonyesha moja ya kitu Madam Lita (katikati), katika mchakato wa kuangalia matokeo ya washiriki hao.
Mshiriki wa shindano hilo Bella Kombo (kushoto), akiteta jambo na Beatrice William, muda mfupi baada ya kuaga mashindano hayo.
Mtangazaji wa kipindi na shindano hilo, Godwin Gondwe, akiwajibika mahari hapo.
Baadhi ya wapiga picha wa shindano hilo wakiwajibika mahari hapo.
Bella Kombo akiwa amemkumbatia Chiby Dayo kwa furaha mara baada ya kutajwa kuendelea kuwemo kwenye shindano hilo.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa kwenye pozi la pamoja na Majaji wao mara baada ya kuhitimisha mchakato huo siku hiyo.
Baadhi ya watazamaji wa kinyang'anyiro hicho wakiwa bize na kuangalia jinsi mambo yalivyokuwa yakiendeshwa mahari hapo.
Madam Lita (kushoto), akiwa kwenye pozi na mmoja wa wadhamini wa mavazi ya washiriki (katikati), na Salama Jabir.
SISTADUU mwenye nembo na element za ‘ki-braza meni’ kutoka jiji lenye miamba la Mwanza Beatice William ‘Brazameni’ ameonja joto la jiwe baada ya kuenguliwa katika mashindano ya kumsaka mwimbaji nyota wa Bongo kataika shindano linaliwajumuisha washiriki wa zamani lenye ‘taito’ ya BSS Second Chance 2011, kwa kigezo cha kupungua kwa kura, MATEJA20 ina full Data.
Tukio hilo lililohuzunisha mashabiki wengi wa mtifuano huo kutokana na swagga za msanii huyo, lilishuhudiwa na MATEJA20, mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam, hali iliyozua majonzi mengi miongoni mwa washiriki hao.
Akizungumza na MATEJA20 muda mfupi baada ya jina lake kutajwa kuenguliwa katika mashindano hayo, Beatrice alisema kuwa japokuwa ameumia lakini hakuna junsi kwani katika mashindano yanayojumuisha watu wengi ni lazima apatikane mshindi mmoja.
“Nikweli nimeumia sana lakini hii ndiyo maana halisi ya mashindano kwamba mwisho wa siku ni lazima apatikane mshindi mmoja” alisema Beatrice.
Aidha, MATEJA20 lilimtafuta mratibu wa shindano hilo, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ kwa lengo la kusikia kauli yake juu ya kutolewa kwa Beatrice ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“kuumia ni lazima sababu mtu kama Beatrice ana kipaji lakini ndiyo hivyo haya ni mashindano ni lazima mshindi awe mmoja” alisema Madam Rita.
Kutoka kwa Beatrice kunabakiza washiriki watano ndani ya shindano hilo ambao ni Rogers Lucas, Chiby Dayo, Bella Kombo, Waziri Salum na Haji Ramadhan.

0 comments:
Post a Comment