Social Icons

Friday, September 30, 2011

LULU AIBWATUKIA MIDUME SABA

Na Erick Evarist
DIVA anayebeba ‘taito’ ya ustaa ndani ya ulingo wa filamu Bongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibwatukia ‘midume’ saba tofauti
anayodai huwa inamsumbua katika simu kila kukicha.
Akizungumza na paparazi wa MATEJA20, hivi karibuni maeneo ya
Leaders Klabu Kinondoni Jijini Dar, Lulu kwa kinywa chake alithibitisha
kuwepo kwa wanaume saba wanaodai ni wakazi wa Mkoani Arusha
ambao wamekuwa wakimsumbua kutaka urafiki wa kimapenzi kila siku
iendayo kwa Mungu.
“Hao jamaa huwa wananikera sababu
hata uwaambie nini huwa
hawaelewi nimeshawaambia kuwa sihitaji urafiki lakini wapi kila kukicha
wananipigia simu.
“Kuna mmoja yeye kila akinipigia ananiambia nimkubalie japo watu
wajue tu ni mpenzi wangu hata kama isipokuwa kweli huku akisisitiza
nikifanya hivyo atanipa mkwanja mrefu a.k.a donge nono la fedha,”
alisema Lulu.
Midume hiyo ambayo mara nyingi imekuwa ikificha majina yao lakini
kwa kipindi kirefu imekuwa ikimsumbua huku wengine wakihitaji nafasi
ya kutaka japo kuonana tu pasipo kufanya lolote la ziada.
Mmoja kati yao akiomba ruhusa ya kumuoa kabla ya kufanya naye jae
tendo lolote lile kama atakuwa tayali maana jamaa huyo anadai
anamzimikia kuliko chochote dunia.


0 comments: