Na Erick Evarist
KIONGOZI wa kruu ya wanaume Family ‘TMK’, Said Fela ‘Mkubwa Fela’ amejitapa kuwa ujio wake mpya wa taarabu ni kuonyesha kuwa yeye si mzugaji katika fani bali ni msanii wa ukweli na mpenda burudani kiujumla.
Akinyetisha habari hii kwa Mateja20, juzikati mkubwa Fela alisema kuwa, tayali ameshakamilisha nyimbo Iitwayo Simuachi aliyomshilikisha Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ na nyimbo hiyo itakuwemo katika albam yake anayotarajia kuitoa hivi karibuni.
Albam na nyimbo hizo amezifanyia kwenye studio yake mwenyewe, ambapo amesema kuwa ananyimbo nyingi za taarab ambazo kawashirikisha wasanii kibao wa muziki huo na kwamba ameamua kufanya hivyo ili kudhihilisha uwezo wake kwa mashabiki.
‘‘Mzigo tayari umekamilika una nyimbo kali ikiwemo Simuachi niliyofanya na Isha Ramadhani na Kimodernmodern niliyoipika na Malikia wa mipasho Bongo Khadija Kopa,’’ alisema Fela huku akimalizia kwa kuongeza kuwa kufuatia maandalizi ya albam hiyo kwa vyovyote italishika jijiji na itafunja rekodi kwa mauzo Kiaani.
0 comments:
Post a Comment