Social Icons

Saturday, September 17, 2011

WANAWAKE WA MADHEHEBU MBALIMBALI DAR, WAFANYA MAOMBEZI YA WALIOPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA MELI YA SPICE ISLANDORSMuongozaji wa ibaada hiyo, akiwa katika sehemu maalum muda mfupi kabla ya maombolezo kuanza.


Akina mama wakiwa katika maombolezo hayo.


Wanawake wa Kiislamu wakiteta jambo wakati wa maombolezo hayo.


…Wakimsikiliza muadhin wa ibada hiyo.


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ghalib Mohamed Bilal, Bi. Asha Bilal akiwasili viwanjani hapo.


Akina mama wa Kikristo wakisikiliza dua hiyo kwa makini.


Msanii wa filamu, Bi. Fatma Makongoro akifuatilia dua pamoja na akina mama wengine.


Mratibu wa dua hiyo ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha Mipango na Uchumi, Mh. Zakia Hamdan Megji akizungumza na akina mama (hawapo pichani).


…Akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.


Mke wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, Bi. Salma Kikwete akiwasili kuhudhuria shughuli hiyo.


Mh. Megji akimkaribisha Mama Salma Kikwete.


Mama Salma akisalimiana na akina mama muda mfupi baada ya kuwasili viwanjani hapo.

Mama Salma (kulia) na mke wa makamo wa rais, Asha Bilal akiwa na nyuso za majonzi.


Mama Salma (kulia), Bi. Asha Bilal na Mh. Zakia Megji wakiwa katika swala maalum.


Mkurugenzi wa The African Stars Entertainment ‘ASET,’ Asha Baraka (kushoto) na mmoja wa akina mama wakifuatilia mawaidha ya kidini.




WANAWAKE wa madhehebu mbalimbali jijini Dar es Salaam, jana jioni waliungana na kufanya maombi na dua maalum kwa ajili ya kuomboleza msiba wa watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya Meli ya MV. Spice Islanders iliyotokea hivi karibuni Visiwani Zanzibar.

Maombolezo hayo yalifanyika kwenye Viwanja vya Karimjee Ilala na kuhudhuriwa na mke wa rais, mkamu wa Rais na baadhi ya wasanii wa filamu


0 comments: