Social Icons

Tuesday, September 27, 2011

AIRTEL YASAIDIA SHULE ZA SEKONDARI TANGA

Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Dr. Ibrahim Msengi akikabidhi sehemu ya vitabu vilivyotolewa na airtel kwa Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Toledo Mwl Soka Basilisa anaeshuhudia ni Afisa Biashara wa Airtel mkoani hapo Bw John Nada na Mwalimu kuu wa shule ya Old Tanga Mwl Kavumo Juma Mzirai katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari Old Tanga Airtel ilitoa ilikabdihi vitabu kwaajili ya sekondari nne sekondari Old Tanga,Tanga Technical, Pande na Toledo mkoani Tanga jana

Wa kwanza kulia ni Afisa biashara wa Airtel mkoani Tanga bw, John Nada akiongea na wanafunzi pamoja na baadhi ya waalimu wa shule za sekondari za Old Tanga,Tanga Technical, Pande na Toledo sekondari (hawapo pichani) wakati ambapo Airtel ilitoa msaada wa vitabu kwa shule hizo, katikati ni mkuu wa shule ya Old Tanga sekondari Mwl Kavumo Juma Mzirai na anaefuata ni mkuu wa Wilaya Tanga Dr.Ibrahimu Msengi aliekuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari Old Tanga jana.


Na mwandishi wetu

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel shule yetu imetoa msaawa vitabu vyenye thamani ya shilingi milion nne kwa shule za sekondani za mkoani Tanga

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Afisa Biashara wa Airtel mkoani Tanga John Nada amesema kampuni ya airtel kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza elimu nchini inatumia sehemu ya faida inayopata na kuirudisha kwa watanzania ili kuboresha huduma za kijamii ambapo hadi sasa imeshatumia zaidi ya shilingi bilion moja kusaidia kuboresha elimu katika nyanja mbalimbali hapa nchini

Shule zinazofaidika na msaada huu hapa mkoni Tanga ni Tanga Technical Sekondari iliyoko Makorora, Old Tanga iliyopo Tanga mjini, Pande sekondari, iliyoko pande njia ya kuelekea Horohoro pamoja na Toledo sekondari iliyoko maeneo Gofu.

Gharama ya vitabu tunavyokabidhi kwa ujumla vinathamani ya shilingi milioni moja kila shule, na vitabu wanavyopata kila shule ni vtabu vya kiada vya English, sayansi, fizikia, na Hesabati, Lengo letu ni kusaidiana na serikali kuinua kiwango cha elimu ya kila mkoa na dio maana tunatoa msaada huu kwenye mikoa yote

Akziungumza wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Dr.Ibrahimu Msengi aliishukuru airtel pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa shule zote zilizofaidika kuvitumia vitabu kikamilifu ili kujiendeleza kwa manufaa ya jamii zao pamoja na taifa kwa ujumla

“Msaada wa Airtel wa Vitabu umekuja wakati shule nyingi za sekondari mkoani Tanga zikikabiliwa na upungufu wa vitabu, hivyo hii itasaidia wanafunzi katika kupata maarifa zaidi kwenye masomo”

Sasa ni jukumu lenu wanafunzi kutumia fursa hii kusoma kwa bidii ili muweze kusaidia taifa baada ya kisomo chenu, msaada huu mkiutumia vizuri ni nyenzo kubwa sana yakusaidia hata faimilia zenu kutokana na faida kubwa mtakayopata kutokana na zao la elimu” alimaliza kusema Dr. Msemi

Wakipokea msaada huo walimu na wanafunzi wa shule za hizo za sekondari Old Tanga,Tanga Technical, Pande na Toledo wamepongeza mpango wa kampuni ya simu Airtel kuwekeza katika elimu na kuomba makampuni mengine kuona umuhimu wa kusaidia katika sekta ya elimu.

Akiongea kwa Niaba ya walimu wakuu wa shule zilizofaidika na mpango wa Airtel shule yetu Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Old Tanga Kavumo Juma Mzirai alisema “ tunawashukuru sana kwa msaada huu wa vitabu ambavyo tunaamini vitatusaidia kuongeza tija katika ufanisi wa kazi zetu pamoja na kusaidia kuboresha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi tunaowafundishia”

Akitoa mfano kuonyesha kiwango cha upungufu ya vifaa vya kufundishia alieleza “Mfano shule ya Old Tanga sekondari inajumla ya wanafunzi wapatao 1,050 ambapo upungufu wa vitabu kwa sasa kuna uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi sita hivyo msaada huu ni dhahiri utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo tulilo nalo pamoja na kuturahisishia kazi sisi waalimu

Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia sekta ya elimu kupitia mpango wake wa Airtel Shule Yetu bado inasaidia shule mbali mbali za sekondari hapa nchini kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za vifaa vya kufundisha pamoja na ukarabati wa majengo ya shule hizo kwa lengo la kusaidiana na serikali kutimiza dhamira ya kuinua kiwango cha elimu kila mahali.

































































0 comments: