Social Icons

Wednesday, September 28, 2011

AIRTEL TANZANIA NA ENGEN PETROLEUM ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI
Kamishna Mohamed Mpinga akionesha stika hizo za aina tatu kwaajili ya magari, pikipiki na bajaji ambazo mwaka huu zinaalama maalum ambazo haziwezi kugushiwa na mtu yoyote.

(kulia), ni Kamishna Mohamed Mpinga akionesha stika hizo tatu kwaajili ya magari, pikipiki na bajaji.Mkuu waMawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano akijaribu kuonyega uhalisia wa stika hizo.
Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (kulia), akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo na Mjumbe wa baraza la Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya Engen, Shaaban Kayungilo, akikabidhi stika hizo kwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani hii leo. Wengine ni Mkuu waMawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya na Mjumbe wa baraza la Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu.
Baadhi ya wanahabari na wadau waliofika kwenye makabidhiano hayo wakifuatilia zoezi hilo kwa makini.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta ya ENGEN kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti namba ya ajali za barabarani nchini.
Leo tumekutana hapa kutangaza wiki ya nenda kwa usalama ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Bukoba. ENGEN Tanzania kampuni ya nishati ya magari nchini Tanzania na Airtel kampuni ya mawasiliano zilikubaliana kuungana na serikali kupitia Baraza la Usalama Barabarani na Jeshi la polisi kuhamasisha jamii kahusu usalama barabarani ili kupunguza ajali.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ENGEN Meneja Bidhaa Jacqueline Kisoka Kupitia SLOGAN ya mwaka huu inayosema “ Usalama barabarani unahitaji uwajibikaji wa kila mtu” ENGEN Tanzania inayofuraha kuwa sehemu ya jitihada za kuokoa maisha ya watu katika jamii yetu na imejitoa kuhamasisha jamii nzima kuzingatia usalama barabarani kama mchango wake katika huduma kwa jamii. ENGEN ni sehemu ya watumia barabara na watumia barabara wengi hutumia bidhaa za ENGEN ndio maana ni mategemeo ya ENGEN kuwa watumia barabara wote wawe salama ili iweze kuwahudumia.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “kwa miaka 3 mfululizo Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabaaarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa. Mchango wetu kwa mwaka huu ni kuchapisha stika na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 2,200 zenye ujumbe wa mwaka huu “Usalama Barabarani unahitaji juhudi za kila moja wetu” .
Matokeo ya ajali za barabarani ni moja ya masuala muhimu kiafya kitaifa. Kila mtumia barabara anahusika awe mwendesha gari, pikipiki au mtembea kwa miguu. Kila mwaka maelfu ya wanaume, wanawake na watoto hufariki kutokana na ajali za barabarani hivyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji kiuchumi. Hii ndio sababu Airtel imejiingiza katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha jitihada hizi”.
Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.

Note:

Umuhimu wa usalama barabarani hauwezwi kupuuzwa, kila siku tunashuhudia ajali nyingi zikisababisha kupoteza maisha, wa Tanzania wengi, uharibifu wa mali nyingi zenye thamani ya mamilioni. Zaidi ya mguso wa kibinadamu utokanao na ajali za barabarani lakini pia maafa na majeraraha yatokanayo na ajali za barabarani zinaleta athari za kijamii na kiuchumi. Kwa mfano takwimu zinaonyesha kuwa wastani wa watu 2,850 wanapoteza maisha kila mwaka katika ajali za barabarani. Takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kwamba watu 3,582 walipoteza maisha huku majeruhi wakiwa zaidi ya 20,000 wakati watembea kwa miguu na wapanda baiskeli wakiwa hatarini zaidi.

Mwaka 2010 katika jumla ya ajali 22,750 gharama au hasara iliyotokana na ajali za barabarani zinakadiriwa kufika bil 363. Hii ni athari kubwa kiuchumi.

0 comments: