Na Erick Evarist DIVA anayebeba ‘taito’ ya ustaa ndani ya ulingo wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibwatukia ‘midume’ saba tofauti anayodai huwa inamsumbua katika simu kila kukicha. Akizungumza na paparazi wa MATEJA20, hivi karibuni maeneo ya Leaders Klabu Kinondoni Jijini Dar, Lulu kwa kinywa chake alithibitisha kuwepo kwa wanaume saba wanaodai ni wakazi wa Mkoani Arusha ambao wamekuwa wakimsumbua kutaka urafiki wa kimapenzi kila siku iendayo kwa Mungu. “Hao jamaa huwa wananikera sababu hata uwaambie nini huwa hawaelewi nimeshawaambia kuwa sihitaji urafiki lakini wapi kila kukicha wananipigia simu. “Kuna mmoja yeye kila akinipigia ananiambia nimkubalie japo watu wajue tu ni mpenzi wangu hata kama isipokuwa kweli huku akisisitiza nikifanya hivyo atanipa mkwanja mrefu a.k.a donge nono la fedha,” alisema Lulu. Midume hiyo ambayo mara nyingi imekuwa ikificha majina yao lakini kwa kipindi kirefu imekuwa ikimsumbua huku wengine wakihitaji nafasi ya kutaka japo kuonana tu pasipo kufanya lolote la ziada. Mmoja kati yao akiomba ruhusa ya kumuoa kabla ya kufanya naye jae tendo lolote lile kama atakuwa tayali maana jamaa huyo anadai anamzimikia kuliko chochote dunia.
MKUBWA FELA ALBAM YANGU YA TAARAB ITAVUNJA REKODI KITAANI
Na Erick Evarist
KIONGOZI wa kruu ya wanaume Family ‘TMK’, Said Fela ‘Mkubwa Fela’ amejitapa kuwa ujio wake mpya wa taarabu ni kuonyesha kuwa yeye si mzugaji katika fani bali ni msanii wa ukweli na mpenda burudani kiujumla.
Akinyetisha habari hii kwa Mateja20, juzikati mkubwa Fela alisema kuwa, tayali ameshakamilisha nyimbo Iitwayo Simuachi aliyomshilikisha Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ na nyimbo hiyo itakuwemo katika albam yake anayotarajia kuitoa hivi karibuni.
Albam na nyimbo hizo amezifanyia kwenye studio yake mwenyewe, ambapo amesema kuwa ananyimbo nyingi za taarab ambazo kawashirikisha wasanii kibao wa muziki huo na kwamba ameamua kufanya hivyo ili kudhihilisha uwezo wake kwa mashabiki.
‘‘Mzigo tayari umekamilika una nyimbo kali ikiwemoSimuachi niliyofanya na Isha Ramadhani na Kimodernmodern niliyoipika na Malikia wa mipasho Bongo Khadija Kopa,’’ alisema Fela huku akimalizia kwa kuongeza kuwa kufuatia maandalizi ya albam hiyo kwa vyovyote italishika jijiji na itafunja rekodi kwa mauzo Kiaani.
SWAHILI FASHION WEEK KUSHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIAKatibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania 'BASATA' Ghonche Materego (katikati), akizindua Logo mpya ya Swahili Week Fashion, ambayo ni maonyesho makubwa Afrika Mashariki na Kati, yakiwa kwenye mwaka wake wa nne yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa tarehe 10, 11 na 12 mwezi wa Novemba 2011 Dar es Salaam, Tanzania wa pili kulia ni mratibu wa maonesho hayo Mustafa Hassanali, akisuhudia zoezi hilo la uzinduzi na wadau wengine. Katibu Mkuu wa BASATA Ghonche Materego (kushoto), akiwa kwenye pozi la pamoja na muandaaji wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali, muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi huo. Logo itakayotumika kwenye maonesho hayo ikionekana baada ya kuzinduliwa. Mratibu wa maonyesho hayo Mustafa Hassanali (kulia), akielezea namna mashindano hayo yatakavyokuwa. Katibu Matendaji wa BASATA, Ghonche Materego (wa tatu kutoka kushoto), akiwa kwenye pozi la pamoja na wahusika wa maonyesho ya Swahili Fashion kwa mwaka huu muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi huo. Ghonche Materego, Mustafa Hassanali (kulia), wakitazama moja ya video ya maonyesho ya Swahili Fashion yaliyopita, na wadau wengine. Katibu Mkuu wa BASATA Ghonche Materego (katikati), akiongea moja ya jambo kwenye uzinduzi huo.
SWAHILI Fashion Week ambayo ni maonyesho makubwa Afrika Mashariki na Kati, yakiwa kwenye mwaka wake wa nne yatafanyika katika Makumbusho ya Taifa tarehe 10, 11 na 12 mwezi wa Novemba 2011 Dar es Salaam, Tanzania.
Swahili Fashion Week 2011 itawaleta pamoja wabunifu 50 wa mavazi na vishaufu kutoka nchi ziongeazo Kiswahili na nchi nyingine mbali mbali kuonesha ubunifu wao wa hali ya juu na kuonesha mitindo mipya ya mavazi.
“Kwa mwaka huu tumekua maradufu kwani tuna jumla ya wabunifu 21 waliobobea kutoka Tanzania, wabunifu 10 wanaochipukia kutoka Tanzania, na waliosalia wanatoka katika nchi mbali mbali duniani na kwa ujumla wao wanakua wabunifu 50, ambao watakao jiunga na watanzania wote kusherehekea miaka 50 ya UHURU wa nchi yetu.” Alisema Mustafa Hassanali, Mwanzilishi wa maonyesho ya Swahili Fashion Week.
Pamoja na kuwa na maonyesho ya ubunifu wa mavazi kutakua na Maonyesho ya Manunuzi ya bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa Tanzania yalioyoanzishwa mwaka 2010, kwa mara nyingine maonyesho haya yatakua kivutio kikuu katika Swahili Fashion Week. Mpaka hivi sasa, maonyesho haya yana washiriki 30 waliojisajili kushiriki, nahii inafanya maonyesho haya kua maonyesho makubwa nchini.
Kama tulivyokua wa kwanza kuanzisha Maonyesho ya mavazi kama haya, kwa mara nyingine tena tanakua wa kwanza kuanzisha tuzo katika sekta hii ya ubunifu Afrika ya Mashariki na Kati. Kusheherekea mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hii ya ubunifu wa mavazi. Kutakua na Mashindano ya Ubunifu wa Fulana ambayo pia ni ya kwanza, kama njia ya kuwashirikisha vijana na vipaji vyao kama njia ya kukuza sekta hii ya familia hii ya wabunifu.
Pia kuna matukio mbali mbali yanayoandaliwa na na yatafanyika kulekea kwenye maonyesho haya ya Swahili Fashion Week. Kwa kuanza kutakua na maonyesho ya mavazi jijini Arusha ambayo ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 8 mwezi Oktoba 2011 kama njia moja wapo ya kupelekea na kusambaza kazi za ubunifu katika mikoa mingine ya Tanzania.
Swahili Fashion week 2011, itakua inarushwa hewani moja kwa moja kupitia tovuti ya www.swahilifashionweek.com kuwapatia fursa wanahabari wa ubunifu duniani kote na kuwajulisha yanayojiri katika ulimwengu wa ubunifu Afrika Mashariki. Maonyesho haya ya moja kwa moja kutoka Makumbusho ya Taifa yatawapatia fursa Watanzania waishio ughaibuni nafasi ya kuunganika na Watanzania wote katika kusheherekea miaka 50 ya UHURU.
“Tukiwa na malengo ya kukuza biashara hii ya ubunifu katika ukanda huu, ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru washirika wetu wote, waliotudhamini katika miaka iliyopita mpaka wakati huu, na pia tungependa kuchukua fursa hii kuhamasisha makampuni na mashirika mbali mbali kujitokeza na kutuunga mkono kwa kudhamini maonyesho haya ya Swahili Fashion Week” Alimalizia Mustafa.
Swahili Fashion week 2011 imedhaminiwa na Nyumba ya Swahili Fashion Week – Hoteli ya Southern Sun, EATV & East Africa Radio, Precision Air, BASATA (Baraza la Sanaa Taifa), Amarula , Ultimate Security, REDDS Original, Image Masters, Global Outdoor ltd, Vayle Springs ltd, Eventslites, Nipashe, Perfect Machinery ltd, Michuzi blog, PKF Tanzania and 361 Degree.
KWA MHARIRI
KUHUSU SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion Week ni jukwaa linalokua kwa kasi sana kwa ajili ya ubunifu wa mavazi na vishaufu kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na bara lote la Afrika kuonesha vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara ndani na nje ya nchi. Hili limelenga kuhamasisha ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kwamba ubunifu wa mavazi ni njia moja wapo ya kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa zitengenezwazo Africa ( Made in Africa concept)
Swahili Fashion week ni jukwaa kubwa la maonesho ya mavazi katika Afrika ya Mashariki na Kati yafanyikayo kila mwaka kwa SASA. Katika mwaka wake wane, Swahili Fashion Week inasherehekea miaka 50 ya Tanzania kwa kukutanisha wabunifu 50 kutoka Tanzania, nchi na dunia nzima nzima kwa ujumla kusherehekea UHURU wake.
Baada ya kuanzisha jukwaa hili linaloonyesha mafanikiao makubwa kwa katika ya sekta hii ya ubunifu. Swahili Fashion week imelenga kuwa maonyesho ya ya ubunifu wa mavazi linaloonekana sana Afrika na kwa ajili yasoko la kimataifa, lililoundwa, kutengenezwa na kujengwa mwaka 2008 na Mustafa Hassanali.
Thursday, September 29, 2011
TANO BORA YA BSS 2nd CHANCE 2011, YAGONGA SHOO NA BENDI YA TWANGA PEPETA BILICANAS Washiriki wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, walioingia kwenye nafasi ya tano bora, wakiwa kwenye pozi na wanenguaji wa Bendi ya African Stars International 'Twanga Pepeta', muda mfupi baada ya kuingia katika Ukumbi wa Bilicanas Club, tayari kwa makamuzi ya pamoja na bendi hiyo.
WASHIRIKI wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011,usiku wa kuamkia leo, walifanya shoo ya pamoja na Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, ambapo walienda kwaajili ya kujifua zaidi kufuatia ugumu wa shindano hilo lililofikia kwenye hatua ya tano Bora. ambayo inamalizika wiki hii na mshiriki mmoja kati ya watano ataaga mashindano na kubaki washiriki wa nne, washiri hao walizama ukumbini hapo muda mfupi baada ya kutoka kurekodi kipindi kinachorusha matukio ya shindano hilo kupitia kituo cha Runinga cha ITV, katika Ufukwe wa Mbaramwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Washiriki walio kwenye Tano Bora ni Bella Kombo, Haji Ramadhan, Chiby Dayo, Waziri Salum na Rogers Lucas.
Wanenguaji wa Bendi hiyo wakitumbuiza jukwaani hapo. Mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta Lilian Tungaraza ‘Lilian Internet’ (katikati), akiwa kwenye pozi na baadhi ya washiriki wa BSS, Haji Ramadhan (kulia), na Rogers Lucas. Waziri Salim (kulia), na Rogers Luicas (katikati), wakiwa kwenye pozi na wanenguaji wa bendi hiyo, Maria Soloma na Phasha Chibby Dayo, Waziri Salim, wakijenga mapozi namna hiyo kwa warembo hao.
Washiri wa BSS, wakiimba jukwaani hapo.
Mshiriki wa BSS, Bella Kombo akiomba kura kwa mashabiki wa bendi hiyo kwa njia ya kuimba.
Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu (katikati), akiwa kwenye pozi na washiriki hao.
Luiza Mbutu (katikati), akiwa katika pozi na washiriki hao.
Mratibu wa shindano la Bongo Star Search Second Chance 2011, (BSS), ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production, Rita Paulsen 'Madam Rita' (kushoto), akiwa katika pozi na mmoja wa washiriki wa shindano hilo Chiby Dayo, muda mfupi baada ya kumaliza kurekodi kipindi hicho katika Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Madam Rita, akimkumbatia chiby Dayo kama ishara ya kumuaga mara baada ya kazi ngumu ya kurekodi kipindi hicho.
Mmoja wa washiriki wa shindano hilo, Waziri Salum (kulia), akiwa amemkumpatia Chiby Dayo huku akiangua kilio baada ya rafiki yake mmoja kati yao kuyaaga mashindano hayo katika zoezi la kurekodi kipindi hicho lililokuwa likiendelea.
Waziri, aliendelea kulia kwa machungu huku akibembelezwa na Chiby Dayo.
Mmoja wa makamera man, waliokuwa wakiandaa kipindi hicho akiwajibika.
Majaji wa shindano hilo, Madam Rita (katikati), Salama Jabir kulia, na Master J, wakifuatilia mpambano huo kwa makini zaidi.
Jaji mkuu wa shindano hilo Madam Rita, akiongea jambo kwenye mchakato huo.
Washiriki walioingia kwenye tano bora wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Watangazaji wa kipindi hicho Godwin Gondwe (kushoto), wakijadiliana jambo na Bob Junior, wakati wa kurekodi kipindi hicho.
Mshiriki wa kinyang'anyiro hicho Bella Kombo, akionyesha uwezo wake wa kuimba mahali hapo.
Bella Kombo, akionyesha uwezo wake.
Bella Kombo, kazini.
Mshiriki wa shindano hilo Rogers Lucas, akikung'uta gitaa mahari hapo.
Chiby Dayo akiwajibika.
Rogers Lucas, akionyesha ulaini wa nyonga yake jukwaani.