Social Icons

Thursday, August 25, 2011

WASHIRIKI WA BSS 2ND CHANCE, NGOMA BADO NZITO

Washiriki tisa waliosalia kwenye shindno hilo, wakiwa katika pozi la pamoja ndani ya fukwe za Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam, jana ambapo walienda kurekodi kipindi cha shindano hilo.
Baachi ya majaji wa shindano hilo, Mastar Jay (kushoto), akibadilishana mawazo na Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni jaji mkuu wa ishu hiyo, Madam Rita.
Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Salah Kaisi 'Shaa' (kushoto), akiwa kwenye pozi na Madam Rita (katikati), sambamba na rafiki yao.
Mapozi yalitawala namna hii.
Mshiriki wa shindano hilo Bella Kombo akiwa kwenye pozi
Bella Kombo akifikilia jambo.
Rogers Lucas, katika pozi
Matangazaji wa Kipindi cha BSS, Bob Junior, akirekodi kipindi hicho.
Mshindi wa shindano la Tusker Project Fame All Stars 2011, Peter Msechu, akiwa kwenye Fukwe za Mbalamwezi Mikocheni jijini Dar es Salaam na mchumba wake.
Sarafina Mshindo akiwa katika pozi
Mary Lucas nae, akiunda pozi mahari hapo.
Beatrice William, akisikilizia jambo pande hizo
Washiriki wa shindano hilo walioingia top ten (nyumba), wakitamburishwa mbele ya waandishi wa habari, juzikati ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip Masaki jijini Dar.
Baadhi ya washiriki hao wakifuatilia kwa makini moja ya mambo yaliyozungumzwa kwenye utambulisho huo.

WASHIRIKI wa kinyang'anyiro cha Bongo Star Search Second Chance 2011, juzikati walisema kuwa, kutokana na washiriki wenzao wanavyozidi kupungua katika shindano hilo ndivyo na mambo yanavyozidi kuwa magum kwa upande wao maana upinzani unaoibuka kila kukicha.

Akizungumza na MATEJA20, mmoja wa washiriki hao alisema kwamba, amekuwa akipata wakati mugum sana kila anapofikilia suala la kuyaaga mashindano hayo hasa akifikilia zawadi iliyotangazwa.
Msanii huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi aliongeza kwamba, tangu walipoingia kwenye 10 bora, ya shindano hilo hadi sasa ushirikiano baina yao umepungua kwa kiasi kikubwa na hiyo ni tofauti na ilivyokuwa awali.
"Ujuwe mwanzo tulipokuwa zaidi ya 15, tulikuwa tukishirikiana kwa kila jambo hasa katika fikila za muziki, yaani kwasasa asikwambie mtu kuna kipindi tulikuwa tunapata hata muda wa kuambiana ni wimbo gani utaimba lakini sasa suala hilo hakuna tena maana kila yeye anawaza kuwa mshindi tu, sipati picha kabisa hasa tutakapo ingia tano bora", Alisema Mshiriki huyo.

MPIGIA KULA MSHIRIKI UMPENDAE KUPITIA NAMBA 15 747, KWA KUANDIKA BSS UNAACHA NAFASI NAMBA YA MSHIRIKI UNAACHA NAFASI KISHA UNATUMA KWA NAMBA HIYO.

0 comments: