


Msanii wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho 'Maya' (kushoto), akikandamiza futari na mtangazaji wa Star TV, Sauda Mwilima .


Mwimbaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ Charles Gabriel ‘Chalz Baba’ (wa pili kushoto), akipata futari na Mwimbaji wa Bendi ya Msondo Ngoma, Hassani Moshi ‘TX Junior’ (kulia), na marafiki zao.

Aunt Ezekiel, nae akipata msosi mara baada ya kuhudumia wageni wake.

WASANII wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Husna Iddi ‘Sajenti’ jioni ya (jana jumatano), waliarika baadhi ya waumini wa dini ya Kiislaam, na kuwaandalia chakula cha jioni (Futari), nyumbani kwao na Sajenti, Sinza Makaburini.
Ishu hiyo ilihudhulia na baadhi ya watu wakiwemo wasanii kutoka tasnia mbalimbali hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment