Social Icons

Friday, August 12, 2011

TANESCO YAJA NA KAULI MPYA KUHUSU UMEME

Meneja wa Mahusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Badra Masood, akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye mitambo ya kufua umeme, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akifafanua zaidi kuhusiana na ishu hiyo Badra alisema kwamba mgao wa umeme utakoma ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
Akielezea mikakati mbalimbali ambayo TANESCO imejiandaa nayo ni pamoja na kukodisha mitambo yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 100, kutoka Kampuni ya Aggreco ya Mombasa Kenya.
Mitambo iliyowasili leo na kazi ya kuifunga inatarajiwa kuanza hivi hivi karibuni.
pia alizungumzia kuhusu ujio wa mitambo hiyo ya Aggreco, ambapo alisema kwamba hii ilikuwa ahadi ya Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni hivi karibuni.
Mipango mingine ya kumaliza mgao wa umeme ifikapo Disemba mwaka huu ni pamoja na kutumia mitambo ya Symbion yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 112, na mitambo ya Jacobsen inayoendelea kufungwa hatua kwa hatua inayoipa Tanesco uhakika wa kumaliza kero ya mgao wa umeme hikaribuni.

Moja ya kontena lenye mitambo ya Aggreco likiwasili leo mchana ubungo jijini Dar es Salaam.

Mitambo ya Aggreko ikishushwa, tayari kwa kufungwa.

0 comments: