Social Icons

Monday, June 6, 2011

UZINDUZI WA AFYA YA UZAZI NA MTOTO JIJINI DAR

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda akiwa katika pikipiki maalum kwa ajili ya kubebea wagonjwa.
Msanii maarufu wa nyimbo za asili hapa nchini, Mrisho Mpoto akiingia uwanjani kwa staili ya aina yake huku akisindikizwa na wanafunzi.
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadj Mponda leo amezindua rasmi afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa, Dk Alberic Kacou.

Lengo kuu la uzinduzi huo ni mpango madhubuti wa serikali wa kudhibiti vifo vya mama na mtoto hasa wakati wa kujifungua.

Katika sherehe hizo kulikuwepo na vikundi mbalimbali vya wasanii vilivyokuwa vikitumbuiza uwanjani hapo.


Msanii kutoka kundi la sanaa Bagamoyo akionyesha jinsi akina mama wanavyopata mateso wakiwa wajawazito huku huduma za hospitali zikiwa mbali na maeneo wanayoishi.

Pikipiki hii ni maalum kwa ajili ya kubebea wagonjwa amabayo inaweza kurahisisha upenyaji na kufika sehemu ambazo ni ngumu kupitika.

Wafanyakazi wa Idara mbalimbali kutoka Wizara ya Afya wakiangalia vikundi vya ngoma katika uzinduzi huo.

Huu ni mfano wa mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimekaribia na hospitali iko mbali anavyoteseka.

Viongozi wa jukwaa kuu wakimpigia makofi Mrisho Mpoto baada ya kuwakonga nyoyo.

Akina mama amabao ni wakazi wa vijijini ambako huduma za kiafya ni vigumu kuwafikia wakitoa nasaha zao kwa mgeni rasmi.

0 comments: