Social Icons

Thursday, June 2, 2011

KIJANA AUAWA, ATUPWA MTO NGERENGERE

Mwili wa marehemu ukitolewa katika Mto Ngerengere eneo la daraja la Mbuyuni kata ya Kihonda mkoani hapa.
Na Dustan Shekidele, Morogoro
KIJANA Moja ambaye hajafahamika jina lake wala sehemu anayoishi ameuawa kikatili na watu wasiojulikana na baadaye wauaji hao kuutupa mwili wake katika Mto Ngerengere eneo la daraja la Mbuyuni kata ya Kihonda mkoani hapa.

Akizungumza na mtandao huu, mwenyekiti wa serikali za mitaa wa Mbuyuni, Ramdhani Hamis Mpoto, alisema kwamba alipokea taarifa toka kwa wananchi wanaolima mboga mboga pembezoni mwa mto huo kwamba kulikuwa na mtu amekufa eneo hilo la daraja.

"Huyu ameuwawa maeneo ya mtaa wa Godesi na huenda wahusika wa mauaji haya walikuja kumtupa kwenye mto ili kupoteza ushahidi. Hata hivyo, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, mwili wa marehemu ulikwama katika moja ya visiki vilivyo kandoya mt. Tumebaini haya baada ya kufuatilia damu toka hapa mtoni mpaka mtaa huo wa Godesi maana njia nzima imetapakaa damu," alisema mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo pia alilaani vitendo vya watu kujichukulia sheria mikononi kwa kutoa roho za wenzao kwa visingizio mbalimbali vikiwemo vya wizi na ugoni

"Ni kweli inauma sana mtu kuibiwa lakini tukumbuke kwamba roho ina thamani kubwa hata kama ni mwizi au mgoni wahusika wangemfikisha kwenye vyombo vya dola husika. Mimi nalaani sana matukio haya ya kuua watu kikatili," aliongeza kusema mwenyekiti huyo.

Mara baada ya polisi kuupoa mwili wa marehemu huyo mwandishi wetu aliushuhudia ukiwa umefungwa kamba miguuni na mikononi huku sehemu ya paji la uso wake ikiwa na majeraha makubwa.

Zifuatzo ni picha za tukio hilo:

0 comments: