Msanii wa filamu ambaye pia ni MC maarufu Bongo, Jaji Khamis ‘Kashi’ (pichani) hivi karibuni amewekwa kiti moto na wazazi wake kufuatia timbwili lililotokea kati yake na mchumba wake aitwaye Muddy.
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilidai kuwa, wazazi wa msanii huyo walifikia hatua hiyo kufuatia wivu alionao kwa mpenzi wake kiasi cha kusababisha migogoro ya mara kwa mara.
“Wazazi wa Kash wamekuwa hawafurahishwi na tabia yake ya kupenda kugombana mara kwa mara na mchumba wake hivyo ili kuunusu uchumba wao wakaona bora wamkalishe chini na kuweka mambo sawa.
“Katika kikao hicho kila mmoja alionekana kuwa na makosa lakini wakaombana msamaha na kutakiwa kusahau yaliyopita,” kilisema chanzo hicho.
Ijumaa lilifanikiwa kuongea na Kash ambaye alikiri kuwekwa kiti moto na wazazi wake na kudai kuwa alikuwa ni ibilisi tu aliyewapitia.
“Ni kweli ila yameisha na tumeanza maisha mengine, sidhani kama itatokea mimi na mpenzi wangu kugombana tena,” alisema Kash.
0 comments:
Post a Comment