Wiki hii kupitia safu hii tunaye sistaduu ambaye ni msanii wa filamu. Licha ya usanii, pia mwanadada huyu amejipatia umaarufu kutokana na kuuza sura kwenye video za mastaa mbalimbali wa muziki hapa Bongo. Anaitwa Agnes Gerald (pichani).
Alizaliwa Aprili 23, 1988 kwenye hospitali ya Mkoa wa Mbeya na akasoma Shule ya Msingi na Sekondari ya Sangu. Hayo ni kwa uchache tu, zaidi kuhusu Agnes, ungana nami katika maswali 10 niliyomuuliza.
M20: Hili zali la kuuza sura kwenye video mbalimbali umelipataje? Kuna mtu yeyote ambaye anakuunganisha na wasanii hawa?
Agnes: Kwanza ni muonekano wangu lakini pia rafiki yangu mmoja alinikutanisha na baadhi ya wasanii hao na wao wakaona nafaa kuwemo kwenye kazi zao.
M20: Inasemekana umetokea kwenye familia ambayo imeiva kidini, wao wanachukuliaje hili suala la wewe kuingia kwenye mambo haya ya kuuza sura tena wakati mwingine kwenye mavazi ya kimitego?
Agnes: Mh! Baba yangu hataki kabisa kusikia mambo ya muziki na niliwahi kukosana naye lakini nalazimisha kwa kuwa ni moja ya ajira.
M20: Mbali na kazi ya kuuza sura, una dili nyingine zinazokuongezea kipato na kuweza kuishi mjini bila wasiwasi?
Agnes: Mimi ni mjasiriamali, nina teksi zangu mbili lakini pia katika siku zijazo nina mpango wa kufungua Super Market.
M20: Vipi ‘outings’ zako, unapendelea kwenda sehemu gani?
Agnes: Napenda sana kwenda Club kujirusha hasa siku za wikiendi.
M20: Kuna za chini chini kuwa umewahi kumlegezea Belle 9, hebu funguka katika hili.
Agnes: Siyo kweli bwana, huu ni mtambo mkubwa, mimi na yule wapi na wapi?
M20: Kabla ya kuanza mechi ya kiutu uzima, unapenda wewe na mpenzi wako muwe katika hali gani?
Agnes: Huwa ‘nainjoi’ sana wote tukiwa tumelewa (Anaangua kicheko).
M20: Ni kipi unachokumbuka katika mapenzi yako ya utotoni?
Agnes: Ni pale nilipokutana kwa mara ya kwanza na mwanamume. Pia nilipobeba ujauzito nikiwa mdogo hali iliyonifanya nifukuzwe nyumbani na baba.
M20: He! Sasa ulijifungua au uliichoropoa mimba?
Agnes: Ilibidi nizae, tena mtoto wa kike, anaishi na baba yake huko Kinondoni ngoja nikuoneshe picha (Anafungua simu na kumuonesha mwandishi).
M20: Dah! Mzuri sana, kwa nini huishi naye?
Agnes: Baba yake amemng’ang’ania kitu ambacho kimenifanya nimchukie mzazi mwenzangu huyo.
M20: Lakini bado unampenda mwanamume huyo?
Agnes: Hapana kwa kuwa baada ya kunipa mimba alinisaliti, wakati nilifukuzwa nyumbani kwa sababu yake, kimsingi sitaki hata kumsikia.

0 comments:
Post a Comment