Na Mussa Mateja
STAA wa tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack’ juzikati aliibuka na kusema kwamba, sasa hawaogopi tena wabunge kama ilivyokuwa huko nyuma.
Jack alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na Ijumaa huku akieleza kuwa, hali hiyo inakuja kufuatia ziara ya bungeni ambayo yeye na wasanii wenzake waliifanya hivi karibuni.
“Huko nyuma kusema ukweli nilikuwa nawaogopa sana waheshimiwa wabunge, nilikuwa nikiwaona kama watu tofauti, watu ‘siriasi’ lakini tulivyoenda kule Dodoma na kujichanganya nao, ile hali imeondoka, kumbe ni watu wanaobadilika kutokana na mazingira wanayokuwa,” alisema Jack.
0 comments:
Post a Comment