Mzee Raza (kushoto) katika pozi na mwanae Eddy kwenye baadhi ya kazi zake.
Mdau (kulia) akimuuliza Mzee Raza maswali kuhusiana na…
Mzee Raza (kushoto) katika pozi na mwanae Eddy kwenye baadhi ya kazi zake.
Mdau (kulia) akimuuliza Mzee Raza maswali kuhusiana na kazi zake.
Salaam,
UTAMADUNI na sanaa ya Mtanzania vimewasisimua watazamaji waliohudhuria maonyesho ya mchoraji Raza Mohammed mjini London siku chache zilizopita. Mzee Raza ameanza kazi ya kuchora picha tokea kipindi cha uhuru mojawapo ya kazi zake ni pamoja na "TINGATINGA", JUMA NA ROZA. Pia amewahi kuwachora baadhi ya viongozi wetu kama Rais Mstaafu Mwinyi, Jakaya Kikwete na wengineo wengi.
Akifungua maonyesho hayo yatakayoendelea kwa mwezi mzima kwa niaba ya serikali, Kaimu Balozi wa Tanzania Uingereza, Mheshimiwa Chibaka Kilumanga alilishukuru shirika la Global Fusion Music and Arts (GFMA) chini ya uongozi wa Louisa Le Marchand kusaidia kutayarisha shughuli hii.
Bwana Kilumanga alisema Raza alialikwa Uingereza awali kusaidia sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Bongo.
Soma zaidi Habari
Habari hii imeandaliwa na Freddy Macha akishirikiana na URBAN PULSE CREATIVE
Zifuatazo ni picha za tukio hilo:
Eddy mwenye kofia akiwa na baba yake Mzee Raza wakiweka picha ukutani.
Kutoka kushoto: Freddy Macha akifurahia Jambo na Baraka wakiwa na wadau wengine.
Freddy Macha (kushoto) akiwa kazini na bendi ya Global Fusion wakiwatumbuiza wadau waliojitokeza kwenye onyesho hilo.
Baaadhi ya kazi za Eddy.
Baadhi ya kazi za Mzee Raza.
Wadau mbalimbali walijitokeza kuangalia kazi za Mzee Raza na mwanae Eddy.
Wadau wakifurahia burudani.
Wadau wakijadiliana jambo.
Wadau wakipata misosi.
0 comments:
Post a Comment