Social Icons

Tuesday, June 14, 2011

GLOBAL SARAKASI YAPAGAWISHA MORO

Picha ya kwanza juu mwanasarakasi wa 4 Boys akizungusha ringi la baiskeli katika sehemu zake za siri.

Picha inayofata wanasarakasi wa 4 Boys wakiendelea kutoa burudani.

KUNDI cha Sarakasi kutoka jijini Dar es Salaam linalojulikana kwa jina la '4 Boys', limeonyesha umwamba wake katika sanaa hiyo baada ya jana usiku kuwapagawasha wanachama wa Klabu ya Sigara 'TTC' tawi la Morogoro kwenye sherehe yao iliyofanyika ndani ya Ukumbi wa Glonens uliopo maeneo ya nane nane mkoani humo.

Hata hivyo, burudani ya kundi hilo nusura ipate dosali baada ya mwanasarakasi mmoja kulizungusha ringi la baiskeli na kulichomeka sehemu zake za siri huku likizunguka kwa muda wa dakika zisizopungua nne, kitendo kilichomkera mmoja wa wanachama wa TCC.

Katika sherehe hiyo, kundi la Wane Stars pia lilikuwa miongoni mwa makundi yaliyotoa burudani. Ilielezwa kuwa, masharti ya kujiunga na uanachama wa TCC ni pamoja na kuwa mvutaji mzuri wa sigara.



mmoja wa wanasarakasi wa 4 Boys akiwa ameruka hewani.
Wakionyesha staili ya sarakasi ya kubebana kwa kichwa.

Wakionyesha burudani ya kuvutana kwa kutumia kamba huku mmoja akiwa hewani.


Staili ya kuruka na kutua kwa kutumia mikono.

0 comments: