Mmoja wa washiriki hao akionesha uwezo wake wa kudansi.
PICHA JUU: Miss Ustawi 2011, Joseline Kombe (katikati), akipunga mkono wa shukurani kwa mashabiki wake, (kushoto) mshindi namba tatu, Catherine Boniface, mwisho kulia ni mshindi namba mbili Diana Bisebo.
SHINDANO la kumsaka mlimbwende wa Miss Ustawi 2011, usiku wa kuamkia leo ulimalizika kwa mbinde ndani ya Ukumbi wa Mawela Pub, Sinza jijini Dar es Salaam, ambapo mshiriki mwenye namba 4, Joseline Kombe alitwaa taji hilo huku akiwabwaga warembo zaidi 11 aliokuwa akichuana nao.
Katika Kinyanganyilo hicho kulikuwa na burudani mbalimbali za muziki kutoka kwa wanafunzi wa chuo hicho na wasanii kutoka Lebo ya Zizzou Entertainments, Edison Wilson ‘Baby Boy’ na Albert Mangwea ‘Ngwea’ walisindikiza kinyang’anyiro hicho.
Waziri wa Utamaduni na Michezo wa Chuo hicho, Songoro, (kulia), akifanya makamuzi na Naibu wake Chibao.
Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Albert Mangwea (kushoto) na Edison Wilson ‘Baby Boy’ wakitumbuiza Ukumbini hapo.
0 comments:
Post a Comment