Social Icons

Saturday, June 4, 2011

FIESTA HAINA MAJOTRO! MISHEMISHE ZA JIJI LA DAR Mhh!


Pichani juu ni Kijana aliyejitambulisha kwa jina la Dulla akimnyonya mdomo nyoka wake, huku umati mkubwaukifuatilia uzinduzi huo wa Serengeti Fiesta 2011 katika viwanja vya Manzese Dar.

Umati mkubwa ulifurika jana mchana maeneo ya Manzese darajani kushuhudia uzinduzi wa Tamasha la Fiesta ambao ulienda sambamba na burudani mbalimbali ikiwemo kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Dulla kucheza na nyoka.

Aidha, usiku lilifanyika shindano la kumsaka Miss Kurasini 2011. Shindano hilo lililowashirikisha warembo 14 lilifanyika katika Ukumbi wa Equator Grill uliopo Mtoni kwa Azizi Ally jijini.


wengine wakiwa juu ya miti


Vijana wakitoa shoo ya nguvu katika uzinduzi huo.


Wanafunzi wa darasa la nne wakipata supu katika ngazi za daraja la Manzese.

Nyumba zikiwa zimebanana eneo la Manzese hii ni hatari kama moto utatokea kwani itawawia vigumu wa wa zima moto kufanya kazi ya uokoaji.


Miss Kurasini 2011, Mwajabu Juma (katikati) akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi.


Mnenguaji wa Kundi la Kanga moja akionyesha umahiri wa kunengua katika shindano hilo la kumsaka Miss Kurasini...'haina majotro

0 comments: