Usiku wa kuamkia leo, katika ukumbi wa Mlimani City, wanahabari bora wa Magazeti, Runinga, Radio, Wapiga Picha na Wachora Katuni walitunukiwa kwa kupewa tunzo na zawadi mbalimbali kwa kuthamini kazi zao nzuri walizofanya mwaka jana. Tunzo hizo za kila mwaka zimeandaliwa na Bararaza la Habari Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na zimepewa jina la Excellence Journalism Awards Tanzania (EJAT). Pichani ni Mweneyekiti Mtendaji wa IPP Media, Bw. Reginald Mengi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi walioshinda sehemu ya tunzo hizo mara baada ya kukabidhi cheti na zawadi.
Mwandishi wa ITV, Festus Sigamonamo (kulia) akipokea tunzo yake kutoka kwa Bi. Fauziat Aboud
Majaji wasataafu wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bi. Blandina Nyoni (kulia)
Bw. Mengi akiwa na Jaji Mstaafu, Mark Bomani
Mtangazaji wa TBC1, Masoud Masoud (kulia) akipokea tunzo yake
Mtangazaji wa Radio Mlimani (Tuma Dandi) kulia, akipokea tunzo yake baada ya kuibuka kidedea
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Bi Joyce Mhaville (kulia) akimkabidhi tunzo mtangazaji Dorcas Raymond wa Channel Ten
Bi. Joyce akiteremka stejini baada ya kukabidhi tunzo
...Dorcas akifurahia tunzo yake
Bosi wa Azam FC, Bw. Mohamed Abeid (kushoto) akikabidhi tunzo kwa mwandishi wa Mwananchi Bi. Sheila
...Mtangazaji wa ITV, Sam Mahela (kulia) naye hakutoka kapa.....
...Sam akiwa na furaha tele baada ya kupongezwa na bosi wake, Mzee Mengi
....Ma MC wa shughuli, Taji Liundi na Chiku Lweno
Mkurugenzi wa Executive Solution , Aggrey Marealle,kushoto, akitoa tunzo kwa mchora katuni bora
..tunzo ya Mpiga Picha bora wa magazeti, ilienda kwa Bashir Nkoromo 'mzee wa chachandu' (kulia) kutoka gazeti la Uhuru na Mzalendo
...mtangazaji wa ITV kanda ya ziwa, Emmanuel Chacha akitoa nasaha zake baada ya kutunukia tunzo ya uandishi bora wa habari za biashara na uchumi..
0 comments:
Post a Comment