Social Icons

Wednesday, May 11, 2011

VODACOM YAZINDUA HUDUMA YA DSTV MOBAILE

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Said Meck Sadiki, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya Dstv Mobile. Huduma hiyo inapatikana kwa wateja wa Vodacom Tanzania kwa kupitia simu za mkononi zenye 3G, ambapo Vodacom na Dstv wameshirikiana kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuweza kunasa na kujua baadhi ya vipindi na ratiza za vipindi za Dstv. Kushoto Meneja Mkuu wa Dstv, Felix Kyengo,Ofisa Mkuu wa kitengo cha uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Corriea.


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Said Meck Sadki (katikati) Meneja Mkuu wa Dstv, Felix Kyengo (kushoto) na Ofisa Mkuu wa kitengo cha uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Corriea, wakionyesha simu zao jinsi huduma ya DSTV Mobile inavyofanya kazi baada ya Kaimu mkuu wa mkoa wa Dares Salaam kuizindua huduma hiyo rasmi.


Mkurugenzi Mkuu wa Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia (kushoto), Meneja wa mambo ya nje wa Vodacom Tanzania, Nector Foya (katikati) wakijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano wa Dstv, Maiyo Simapungula, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya DSTV Mobile.



Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam Said Meck Sadiki (wapili kushoto) akijadiliana jambo na Meneja Mkuu wa Dstv,Felix Kyengo (kushoto) baada ya uzinduzi huo. Kulia ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha uendeshaji wa Vodacom Tanzania Peter Corriea na Mkuu wakitengo cha huduma za mtandao wa mawasiliano wa kimataifa wa Vodacom Tanzania Candice Rato.

0 comments: