Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Mbweni JKT, Mwanaidi Hassan (kulia) akipewa tuzo na Makamu wa Rais baada ya kuibuka mchezaji bora pamoja na kupewa zawadi ya gari aina ya Toyota Crester.
Chama wa Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) jana kiliwakabidhi zawadi wanamichezo mbalimbali wa hapa nchini wanaocheza nje ya nchini na wageni wanaocheza hapa nchini. Katika shughuli hiyo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Dk.Ghalib Bilal na kuhudhuriwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
Makamu wa Rais (kulia) akimpa tuzo ya heshima, Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kutokana na mchango wake mkubwa katika michezo hususan ujenzi wa Uwanja wa Taifa.
Mkapa akiwashukuru TASWA kwa kukumbuka mchango wake.
Mwanaidi akiwa ndani ya gari lake baada ya kukabidhiwa na Dk. Bilal
Mwanaidi akiwapungia mkono wageni waalikwa.
Dk. Bilal, Mkapa na wageni wengine waalikwa wakifurahia jambo ukumbini hapo.
0 comments:
Post a Comment