Mgeni rasmi wa utamburisho huo, Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kushoto), akiongea jambo kwenye utambulisho huo, (katikati) ni mratibu wa shindano hilo Maimartha Jesse na Dominic Nyalipha.
UTAMBULISHO wa Shindano la kumsaka Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, linaloratibiwa na Mmiliki wa Duka la Manywele, Maimartha Jesse na uongozi wa bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, usiku wa kuamkia leo umefana vilivyo ndani ya ukumbi wa Sun Cirro Club, Shekilango jijini Dar es Salaam, baada ya mashabiki kibao kujitokeza kushuhudia shoo hiyo.
Baadhi ya Vimwana Manywele Twanga Pepeta, waliowahi kushiriki shindano hilo wakitoa shoo ya utangulizi kabla ya washiriki wa mwaka huu kupanda jukwaani.
Baadhi ya wanenguaji wa African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Asha Saidi ‘Sharapova’ (kushoto), akipiga picha katika shoo hiyo akiwa na mwenzake Lilian Tungalaza ‘Lilian Internet’.
Mmoja wa washiriki wa Kimwana Manywele Twanga Pepeta 2011, Laitiness Mshana akionyesha uwezo wake.
Mshiriki wa shindano hilo Mary Hamisi, akitambulishwa ukumbini hapo.
Vimwana hao wakitoa shoo ya utambulisho jukwaani hapo.
Kimwana Manywele Twanga Pepeta, Amina Juma akionyesha umahiri wake jukwaani.
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya 20% (wa pili kulia), akifanya makamuzi kwenye utambulisho wa Kimwana Manywele Twanga Pepeta na wasanii wenzake.
0 comments:
Post a Comment