Fatma Abdallah (Fetty) akiongea jambo kwa wanahabari.
WASHIRIKI wa kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Dar City Centre 2011, watamenyana vikali ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar es Salaam, Ijumaa wiki hii.
Akizungumza katika ukumbi wa Hoteli ya Lamada mapema leo, Mratibu wa shindano hilo, Fatma Abdullah (Fetty) alisema hadi sasa kuna washiriki 18 ambao watagombea taji hilo.
Aliongeza kwamba washiriki wote hao wana sifa za kushinda, jambo ambalo anaamini litawapa wakati mgumu majaji wa shindano hilo.
“Hata wakibahatika kwenda kuwania taji la Miss Ilala naamini taji hilo litabakia hapa,” alisema.
Akiongelea maandalizi ya shindano hilo, Fetty alisema mambo yote yako tayari kinachosubiriwa ni muda wa shimdano hilo na kwamba tiketi za VIP zitakuwa ni 30,000/= na za kawaida ni 15.000/=.
Katika hafla hiyo bendi za African Stars International ‘Twanga Pepeta’ na Tip Top Connection, zitatumbuiza.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio mbalimbali kwenye kikao hicho.
Warembo husika wakibadilishana mawazo na mratibu baada ya kikao kumalizika.
0 comments:
Post a Comment