DOA jeusi la ajali za barabarani zinazowahusisha waendesha pikipiki nchini linazidi kukua kutokana na wahusika kutozingatia sheria za barabarani ambapo Jumatatu mwendesha pikipiki aliyejulikana kwa jina moja tu la George alikufa baada ya kuingia uvunguni mwa lori la Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Shuhuda wa ajali hiyo aliyejulikana pia kwa jina moja tu la Joshua, aliuambia mtandao huu kwamba marehemu aliyekuwa amempakia abiria wa kike alijaribu kulipita lori hilo lenye namba za usajili SM 3365 lakini akashindwa na kujikuta ameingia katika uvungu wake na hivyo kuanguka vibaya katika barabara ya Morogoro-Dodoma.
“Alianguka chini baada ya suruali yake kunasa pembeni kwa lori hilo ambapo abiria wake alinusurika kwa kutupwa pembeni,” alisema shuhuda huyo akiongeza kwamba Wasamaria wema walimpigia simu ndugu yake kumjulisha juu ya tukio hilo na wakampeleka hospitali haraka, lakini alifariki muda mfupi baada ya kumfikisha mapokezi.
Zifuatazo ni picha za tukio hilo:
0 comments:
Post a Comment