Social Icons

Friday, May 6, 2011

BABA WA PANCHO MWAMBA AFARIKI DUNIA


MUIMBAJI wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Patcho Mwamba (pichani), juzikati alipata pigo la kuondokewa na baba yake mzazi, mzee Valentine Lukusa Makadi, Ijumaa linakuhabarisha.


Kifo cha mzee huyo kilitokea alfajiri ya kuamkia Mei 3, mwaka huu nchini Congo nyumbani kwake alipokua anaishi baada ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali kutokana na uzee aliokuwa nao.

Akizungumza na Ijumaa juzi, Patcho alisema kuwa, hakuna ugonjwa mkubwa uliomuondoa duniani baba yake zaidi ya utu uzima.

“Hakuna ugonjwa uliokuwa ukimsumbua baba zaidi ya utu uzima wake, kweli ni pigo kubwa kwangu kutokuwa na mtu muhimu niliyependana naye na kumtegemea kwa kila kitu, lakini kwa upande mwingine ni mapenzi ya Mungu,” alisema Patcho kwa masikitiko.

Hata hivyo, hakuweka wazi ni lini ataanza safari kuelekea nchini Kongo kuhani msiba.

0 comments: