Social Icons

Monday, May 16, 2011

KIBAKA ACHEZEA KICHAPO CHA MWAKA MORO

Kibaka aliyejulikana kwa jina la Hassan Maulid mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam, akipokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya jaribio lake la kutaka kuiba baiskeli iliyokuwa imeegesha katika eneo la benki ya CRDB mtaa wa Masika mkoani Morogoro kukwama leo asubuhi.
NA DUNSTAN SHEKIDELE, MOROGORO
KIJANA mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Maulid (29) mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam, leo asubuhi alinusulika kifo baada ya wananchi wenye hasira kali kumshushia kipigo kikali baada ya kukamatwa akitaka kuiba baiskeli iliyokuwa imeegesha katika eneo la benki ya CRDB mtaa wa Masika mkoani hapa.

Mwandishi wetu ambaye alikuwa ndani ya benki hiyo anaeleza kuwa, mteja mmoja aliyekuwa kwenye foleni alimshuhudia kibaka huyo akijaribu kuiba baiskeli yake na baaada ya kuona hivyo alitoka kasi ndani ya benki huku akipiga mayowe ya mwizi ambapo askari waliokuwa wakilinda benki hiyo waliungana nae kumfukuza kibaka huyo.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya, kibaka huyo aliamua kuitupa baiskeli hiyo na kujaribu kuingia ndani ya msikiti wa Kingo lakini malengo yake yalikwama kwa sababu milango ya msikiti huo ilikuwa imefungwa. Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya kibaka huyo aliamua kuingia ndani ya choo cha Mama Lishe aliyekuwa akifanya biashara zake nyuma ya msikiti huo.

Mwandishi wetu alishuhudia kundi la wananchi wenye hasira wakivunja mlango wa choo hicho na kumchomoa kibaka huyo na kuanza kumuangushia kipigo kikali.

Juhudi za askari pamoja na Msamalia mwema mmoja (aliyevaa shati nyeupe iliyotapakaa damu pichani chini) za kutaka kumuokoa kibaka huyo asiendelee kupata kipigo toka kwa wananchi hao wenye hasira ziligonga mwamba kwani walizidi kumpa kisago hadi kuwa nyaka nyaka.

Alipohojiwa na mtandao huu mara baada ya kufikishwa katika maeneo ya usalama kibaka huyo alikiri kutaka kuiba baiskeli hiyo na alikuwa na haya: "Mimi naishi Dar kwa hapa Moro nimefikia maeneo ya Manzese kwa rafiki yangu ambaye nilikuwa naye katika tukio hili, njaa ndiyo iliyotusukuma kutaka kuiba baiskeli hiyo ila naomba mnisamehe sitarudia tena jamani."

ZIFUATAZO NI PICHA ZA TUKIO HILO:

0 comments: