Mh. Idd Azzan akiongea na wanafunzi kabla hajakabidhi meza hiyo.
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni (CCM) Idd Azzan, leo amekabidhi msaada wa meza ya maabara katika Shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya ahadi zake alizotoa katika shule hiyo.
Akiongea kabla hajaenda kukabidhi meza hiyo, mbunge huyo alisema kwa muda mrefu alisikia kilio cha wanafunzi wa shule hiyo kuhusu vifaa vya maabara hivyo kwa kuanzia tu ametoa meza yenye vifaa vya maabara yenye thamani ya shilingi milioni 5,950,000/=.
Naye mkuu wa shule hiyo, Bi Gaudencia Kimario, alimshukuru Azzan kwa msaada wake huo na kumwomba ashughulikie swala la hati ya jengo, umeme na komputer ambapo alikubali ombi hilo na kuahidi kulishughulikia mara
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza.
Akiizindua rasmi.
Kikundi cha ngoma shuleni hapo kikitoa burudani.
0 comments:
Post a Comment