STAA wa mpira wa kikapu, duniani akicheza katika Ligi ya NBA nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka ‘Super Tall’ (pichani) amefanya kufuru ya fedha baada ya kumwaga fedha ukumbini na kuwaacha watu wagombanie, twende mstari kwa mstari.
Paparazi wa gazeti hili lenye heshima ya nyota tano kwa habari za mastaa Bongo, alishuhudia tukio hilo live wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, jijini Dar es Salaam ambapo handsome boy anayecharaza fimbo katika muziki wa kizazi kipya, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ alikuwa akipiga shoo babkubwa.
Awali kasuku wa gazeti hili alimshuhudia Hasheem akikatiza kwa madaha ukumbini humo, akiwa ameongozana na wapambe wake waliokuwa wakimuandalia njia, kisha kukaa sehemu moja na kuanza kula bata kwa mtindo wa ‘tingisha kama imeisha, leta nyingine’.
Wakati shoo ikiendelea Hasheem aliinuka na wapambe wake kuongoza mbele kama kawa, kisha wakaelekea jukwaani alipochomoa burungutu moja la ‘nyekundu nyekundu’ tupu na kumkabidhi Dully Sykes ambaye aliongeza manjonjo baada ya kutuzwa na supastaa huyo.
Hakuishia hapo, aliposhuka jukwaani, alizama mfukoni na kutoa burungutu lingine kisha akalirusha juu na mashabiki kuanza kugombania.
Wakati watu wakiendelea kukanyagana wakigombea mkwanja huo wa ‘sadakalawe’ Hasheem na wapambe wake walitoka nje na kuingia kwenye gari aina ya Hummer na kuondoka kiwanjani hapo.
“Duh! Ebwana ee, jamaa huyu ni noma yaani minoti yote hiyo kaiachia watu wanyang’anyane? Hii ni kufuru, kweli mshkaji fedha imemkubali,” alisika jamaa mmoja akisema ukumbini hapo.
Hasheem Thabeet amerejea nchini hivi karibuni akitokea Marekani anapoishi, yupo kwa mapumziko mafupi. Ni Mtanzania pekee anayeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye ligi ya NBA ya mpira wa kikapu nchini humo.
1 comments:
ndo maana anafeli mpira wa kikapu, mambo ya kipuuzi haya
Post a Comment